Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Serikali imewaagiza watu wote wanaofanya shughuli za ujangili kuacha mara moja na watafute kazi nyingine ya kufanya kwani kwa sasa huko porini hakukaliki na Serikali itawasaka popote pale walipo hata kama ni nje ya Nchi na kuwakamata watu wote wanaofanya ujangili bila kujari cheo cha mtu na .
Agizo hilo la Serikali lilitolewa hapo jana na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof Jumanne Mghembe wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya ukakamavu kwa Wahifadhi wa Wanyama Pori kutoka Tanapa , Mamlaka ya Ngorongoro na Tawa yaliofanyika katika kituo cha mafunzo cha Mlele Mkoani Katavi .
Alisema agizo kwa majangili wanaofanya ujangili waache kufanya kazi hiyo na watafute kazi nyingine ya kufanya kwani Serikali itawasaka huko huko waliko hata kama ni nje ya Nchi na wala hawata jari i cheo cha mtu na wajukuwe kuwa sasa hivi porini hakukaliki tukana na Wizari ilivyojizatiti katika kulinda rasimali za nchi .
Waziri Mghembe alieleza katika kipindi cha mwezi Agosti hadi Oktoba mwaka huu majangili 107 walikamatwa hapa Nchini wakiwa na nyara mbalimbali za Serikali pamoja na silaha kutokana na kuwepo kwa uporesheni Faru
Alisem Serikali itaendelea kutekeleza mkakati wa Kitaifa wa kupambana na ujangili na biashara haramu ya wanyama na nyara za Serikari National Strategy to Combat Poaching and lllegal wildlife Trade pamoja na mambo mengine mkakati unataja umuhimu wa kuwapatia mafunzo wahifadhi wanyama pori yatakayo wawezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi .
Jitihada zitaendelea kufanyika na kuhakikisha kwamba kila furusa ya mafunzo inayopatikana inatumika vizuri ili kuwajengea uwezo watumishi kwa kuwapatia mbinu za teknojia ya kisasa katika kupambana na ujangili .
Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kushirikisha wadau mbalimbali kutoa mafunzo ,vitendea kazi na teknojia ya kisasa itakayorahisisha kuwabaini na kuwakamata majangili ndani au nje ya maeneo yaliyohifadhiwa .
Alisema sekta ya Uwifadhi imeanza kutumia ndege zisizo na rubani DRONES kubaini majangili katika baadhi ya maeneo ya hifadhi hapa nchini na matumizi ya mbwa wa kunusa katika kufutilia majangili na katika ukaguzi wa nyara za Serikali .
Alieleza kuwa maeneo mengi ya hifadhi yanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo ujangili hususani wa Tembo , uingizaji wa mifugo hifadhini ,uvamizi wa mipaka ya hifadhi na uwelewa mdogo wa wananchi .
Nae mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa Mtango Mtahiko alisema Tanapa wamekuwa wakifanya kazi kwa kutekeleza maagizo ya Wizara ya Maliasili na Utalii na watendelea kufanya hivyo ili kulinda uhifadhi wa Nchi .
Kaimu Mkurugenzi wa TAWA Martini Loibooki alisema mafunzo hayo waliopatiwa Wahifadhi hao yanaumuhimu mkubwa sana kwani wao ndio wasimamizi wa askari na watahakikisha watumishi wote wa Tawa wanapatiwa mafunzo kama hayo kwani yanawaongezea ukakamavu na uwezo wa kupambana na majangili .
MWISHO
0 comments:
Post a Comment