Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kawanzige katika Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wanalazimika kutumia chumba kimoja cha darasa zaidi ya wanafunzi wa madarasa mawili kwa ajiri ya kufundishiwa masomo kwa wakati mmoja kufutia shule hiyo kukabiliwa na uhaba mkubwa wa upungufu wa madarasa huku wanafunzi wengine wakiwa wanasomea chini.
Kilio hicho cha wanafunzi wa madarasa zaidi ya mawili kusomea katika chumba kimoja kwa wakati mmoja kilitolewa hapo juzi na Diwani wa Kata ya Kakese Mh Maganga Salaganda wakati wa kikao cha Baraza la madiwani wa Manispaa ya Mpanda kilichofanyika katika ukumbi wa Mnspaa hiyo .
Alisema shule ya Msingi ya Kawanzige ambayo ipo kwenye Kata yake inakabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa madarasa hari ambayo inaifanya shule hiyo yenye Wanafunzi wa kuanzia darasa la awali hadi la saba wanafunzi kutumia darasa moja kwa ajiri ya masomo wanafunzi wa madarasa zaidi ya mawili na wote wamekuwa wakifundishwa kwa wakati mmoja .
Aliiambia Baraza hilo la Madiwani lilikuwa likiongozwa kwenye kikao hicho na Meya wa Manispaa ya Mpanda Willy Mbogo kuwa shule hiyo yenye Wanafunzi zaidi ya mia sita inayo madarasa manne tuu.
Hivyo kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa wamelazimika kutoyachukua madawati ambayo yamechangwa na wananchi kwa kuwa hakuna vyumba vya madarasa vya kuyahifadhia madawati huku baadhi ya wanafunzi wakiwa wanasomea chini.
Afisa Elimu wa Manispaa ya Mpanda Vicenti Kayombo alikiri kuwepo kwa tatizo la upungufu mkubwa wa madarasa kwenye shule hiyo.
Alifafanua kuwa mahitaji ya shule hiyo ni madarasa 24 lakini yaliopo hadi sasa ni madarasa manne hivyo shule hiyo inaidadi ya upungufu wa madarasa ishirini.
Katika mwaka huu wa fedha wa 2016 na 2017 Manispaa hiyo imetenga fedha kwa ajiri ya ujenzi wa vyumba tisa vya madarasa na kati ya vyumba hivyo viwili vitajengwa katika shule hiyo ya Msingi Kawanzige hivyo inabakiwa na upungufu wa vyumba 18 vya madarasa.
Kayomba aliwataka Madiwani wa Manispaa hiyo waendelee kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu , matundu ya vyoo na madawati .
Nae Diwani wa Kata ya Makanyagio Haidari Sumry alilalamikia kitendo cha madiwani wa Manispaa hiyo kutokuwa na ofisi zao kwenye Kata wazoziongoza .
Alisema badala ya shughuli zao za kuwahudumia wananchi kuzifanyia ofisini wanalazimika shughuli hizo kuzifanyia kwenye nyumba zao kitu ambacho sio sahihi.
Ajibu hoja ya Diwan huyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda John Nzyungu alisema watajitahidi kukamilisha ujenzi wa ofisi za madiwani kwa awamu awamu kwani manispaa hiyo haina uwezo wa kukamilisha ujenzi wa ofisi hizo kwa wakati mmoja
0 comments:
Post a Comment