Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma .
Katavi
WANACHAMA wa CUF mkoani Katavi wametangaza kuwa hawamtambui Profesa
Ibrahim Lipumba kama mwenyekiti halali wa chama hicho.
.
Msimamo huo wa wanachama hao wa CUF ulitangazwa na Mwenyekiti wa
CUF wilaya ya Mpanda mjini , Alam Ndimubenya katika mkutano na
waandishi wa habari uliofnyik mjini hapa leo.
Alisisitiz kuwa mwenyekiti wa CUF katik ngazi ya wilaya iliyoko
mjini anatambulika kama mwenyekiti wa mkoa husika .
Akifafanua alieleza kuwa mkutano mkuu wa dharura ulitishwa na CUF ,
Agosti 21, mwaka huu ukiwa ajenda mbili ikiwemo ya kuridhia Prof
Lipumba kujiuzulu Uenyekiti wa Taifa wa chama hicho .
“Ajenda nyingine ilikuwa uchaguzi wa Mwenyekiti , Makamu Mwenyekiti
wa Taifa na wajumbe wanne wa baraza kuu la uongozi wa CUF
Taifa…. Lakini baadhi ya wajumbe wachache walimuingiza kwa nguvu
Profesa Lipumba na kufanya fujo iliyosababisha mkutano huo
kuvunjika” alieleza .
Aliongeza kuwa wajumbe hao wachache walifanya vurugu hiyo baada ya
wajumbe 476 wa mkutano huo mkuu wa dhrura sawa na asilimia 70 ya
akidi walilidhia kujiuzulu kwa Profesa Lipumba.
“Wananchi wamekuwa wakizungumza tofauti na iliyokuwa kwa
kutoelewa mamlaka ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa hatua yake
ya kumtambua Profesa Lipumba kama mwenyekiti wa CUF Taifa… basi ni
vema waelewe kuwa mamlaka yake yanishia katika kuvisajiri vyama
vya siasa na si vinginevyo “ aliongeza kusema .
Alisema kuwa sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya 1995 toleo la
2015 ikieleza wazi katika kifungu cha 20 juu ya mamlaka ya Msajili
wa Vyama vya Siasa kwamba yanishia katika kuvisjili vyama vya
siasa.
Hivyo wanamuomba msajili wa vyama vya
siasa asijiengize kwenye mambo ya CUF kwani matatizo ya CUF
yatawalizwa na wanachama wenyewe wala si Msajiri wa vyama vya siasa.
alisema Mwenyekiti Dimubenya
Mwisho
0 comments:
Post a Comment