Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Msakila, Manispaa ya Mpanda mkoani
Katavi , Didas Makona ameaapa kuwa endapo shule yake ispokuwemo
kwenye kumi bora ya shule zitakazoongoza Kitaifa katika matokeo
ya Kitaifa ya kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka huu , atajiuzulu kwa
hiyari wadhifa wake .
Akisisitiza kuwa itakuwa fedheha kubwa kwake na haoni sababu kwa
nini shule yake hiyo ishindwe kuwemo kwenye orodha ya shule za
msingi kumi bora katika matokeo ya Kitaifa ambayo yanatarajiw
kutangazwa baadae mwaka huu.
Mwalimu huyo alijigamba hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari leo , ofisi kwake shule hapo katika Mtaa wa Kawajense ,
Manispaa ya Mpanda ..
Nimekuwa Mwalimu Mkuu wa shule hii kwa miaka mitatu sasa
nimewajengea misingi mizuri kielimu wanafunzi wanaosoma katika
shule hii ambao wana nidhamu ya hali ya juu …..” alisisitiza .
Akifafanua alieleza kuwa mwaka 2012 ufaulu wa kuhitimu elimu ya
msingi katika shule hiyo ulikuwa asilimia 52 .
“Mwaka 2013 nilihamia katika shule hii na ufaulu ulikuwa
asilimia 76 mwaka 2014 asilimia 92 na mwaka jana ufaulu
ulikuwa aslimia 100…… kwa matokeo hayo mwaka jana kimkoa shule hii
ilishika nafasi ya kwanza huku kitaifa ilikuwa ya 200 “
alisisitiza
Alisisitiza haoni sababu itakayo ifanya shule hiyo kutokuwa kuwa
kwenye kumi bora kutokana na jinsi ambavyo amewaandaa wanafunzi
wake 76 waliohitimu elimu ya msingi mwaka huu..
Sababu nyingine aliitaja kuwa ni uwezo waliokuwa nao wanafunzi
wake katika masomo ya Hisabati na Kingereza ambapo kwenye
mitihani sita ya majaribio iliofanyika kimkoa robo ya wanafunzi
76 walipata alama A ya ufaulu , huku waliobaki wote walipata
alam a B wanafunzi wake robo ya darasa wamekuwa wakipata alama B
ya ufaulu..
Alitamba kuwa mtihni huo wa mjaribio wanafunzi hutumia dakika 45
kufanya masomo hayo ya Hisabati na Kingereza huku muda wa
kitaifa ni saa mbili huku akisisitiza kuwa wanafunzi waliohitimu
daras la saba mwaka huu walikuwa wakijitungia maswali wenyewe na
kutafuta majibu wenyewe .
.Alisema uwezo huo walioonesha ni vigumu sana kufanywa na
wanafunzi kwani kazi hizo zimezoeleka kufanywa na walimu wao
Afisa Elimu wa Manspaa ya Mpanda Vicenti
Kayombo alisema mwalimu Mkuu huyo alishafika ofisini kwake na
alimwomba amvue wadhifa wa ualimu Mkuu indapo shule hiyo
haitakuwa kwenye shule kumi bora kitaifa na amwamishe kwenye
shule hiyo na kumpangia kituo kingine cha kazi huku akiwa ni
mwalimu wa kawaida..
Mwisho
0 comments:
Post a Comment