Katavi
Mkuu
wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando amevunja bodi ya chama cha
ushirika wa wakulima wa tumbauku mishamo kuagiza kukamatwa kwa
viongozi wa bodi, mkandarasi aliyehusika kupewa kandarasi ya kupanda
miti, Afisa Ushirika,kamati ya miti ya mkoa na wale wote waliohusika na
upotevu wa fedha zaidi ya shilingi milioni 142 zinazodaiwa kupotea kwa
kumlipa mzabuni alipewa zabuni ya kupanda miti kati kampuni ya Mtuka
Investment inayomilikiwa na Moses Christopher Fred kwa ajili ya Kupanda
miti 3,25000 yeye alipanda miti 74,000 tu katika vijiji vya Tarafa ya
Mishamo kwa ajili ya wakulima watumbaku mishamo, Mkoani Katavi.
Mkuu
wa Wilaya alifikia hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa
wakulima tumbaku wa Tarafa ya Mishamo kuhusu ushirika wao wa wakulima
wa Tumbaku TAMCOS viogozi kutuhumiwa kuwadhurumu wakulima kwa kuwakata
fedha za mauzo ya zao la tumbaku na kumlipa mkandarasi ambaye
hakutekeleza wajibu wake ipasavyo.
Kufuatia
kupokea malalamiko hayo Mkuu wa wilaya aliunda tume iliyopita kuhesabu
miti kwa kila kijiji kilichoelezwa kuwa miti ilipandwa kumbe
haikupandwa,ililipwa miti hewa,hivyo katika mkutano wa hadhara
uliofanyika mishamo mkuu wa wilaya alitoa maamuzi kuhusu malalamiko ya
wakulima hao.
Akifafanua
Zaidi alisema kuwa kazi aliyowaahidi wananchi kuwa atahakikisha kazi
anaifanya kuona jasho la munyonge halipoei.amlisema hela iliyokuwa
ikilalamikiwa na wananchi ilikuwa shilingi milioni 142.iliyolipwa kwa
mkandarasi mtuka kwa kupanda miti ambayo haipo.
Akizungumza
kuhusu afisa ushirika ambaye ndiye jicho lake la kwanza
alipomwulizakuhusu kama miti imepandwa kwa kuwa anasikia harufu ya wizi
kuhusu upandaji miti kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2014/2015 chama cha
ushirika tamcos,pia akamwagiza kushughulikia malalamiko ya pesa za
masawazisho hakuweza kumpatia majibu ya kuridhisha.
Kufuatia
malalamiko hayo akaagiza kukamatwa kwa Mkandarasi husika mtuka
Investment,bodi ya chama cha ushirka mishamo,Kamati ya Miti na Afisa
ushirika na kuwataka fedha zilizopotea shilingi milioni 142 zirejeshwe
baada ya hapo Taasisi ya kupambana na Kuzuia Rushwa Kwa kusirikiana na
Jeshi la polisi wafanye uchunguzi na ili iwapo watabainika na makosa
wapelekwe mahakamani kufunguliwa mashitaka.
kuhusu
bodi ya ushirika wa wakulima wa tumbaku mishamo amesema kwa mazingira
hayo amezungumza na mkuu wa mkoa huo Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga
kuivunja bodi ya ushirika wa wakulima wa tumbaku Mishamo kisha iundwe
bodi mpya ndani ya wiki moja itakayoweza kuwahudumia wakulima wote.na wale wakulima waliokuwa wamefukuzwa katika ushirika huo warejeshwe na kuendelea na shughuli zao kilimo.
Kwa
upande wao Sief Elias Mbazimtima, Sesilia Emanuel , Mbonele, Emanuel
Gabriel Wakabanga, wanachama wa chama cha wakulima wa tumbaku na
wananchama wa TAMCOS kwa nyakati tofauti wameeleza kukubaliana na
maamuzi yaliyotolewa na mkuu wa wilaya kuhusu kuvunjwa bodi na kukamtwa
wa viongozi wa TAMCOS kuwa ni uamuzi wa busara sana.
Mwingine
akaenda mbali Zaidi wamenyonywa muda mrefu lakini sasa kilio chao
kimefikia mwisho kwa kuwa wamekuwa wakilima “Tunashukuru sana kwa kuwa
tumekuwa tukinyonywa kwa muda mrefu kila tukilima hatupati fadia na
hatukupata mahali pa kukimbilia lakini serikali ya awamu ya tano imeweza
kuwasaidia kilio chetu alisema Mmoja wa wakulima hao”.Emanuel Gabriel
Kabanga.
Awali
katika Mkutano huo wa hadhara Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya
Mpanda Hamed Mapengo aliomba wawe watulivu pia akawataka wawe wasikivu
kuusiana na majibu yaliyotolewa akawataka wakulima hao wa zao la tumbaku
kutatua kero zao ambazo amezipata na kuzifanyia kazi .
Na
asilimia kubwa ya wakazi wa wilaya yam panda wanatengemea zao la
tumbaku laikini wakulima wamekubwa na changamoto kubwa ya umasikini
pamoja na kuwa wanalima tumbaku ambalo ni zao linalotegemewa na
halimashauri kuwaingia fedha na hata halmashauri inategemea sana mapato
kutoka zao la tumbaku kama ushuru amBAPO Halmashauri ya Mpanda inapata
mapato makubwa kutokana na zao la tumbaku.
0 comments:
Post a Comment