Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imewaukumu watu wawili Godfrey Mabuga na Rashid Ramadhani wakazi wa Mtaa wa Nsemlwa Mjini hapa kutumikia kifungo cha jumla ya miaka 40 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukamatwa na Meno ya Tembo yenye thamani ya shilingi milioni 48.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi uluotolewa na upande wa mashitaka kwenye kesi hiyo.
Awali katika kesi hiyo mwendesha mashitaka mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi Jamira Mziray alidai washitakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo hapo Mei 20 mwaka 2014 huko katika eneo la mtaa wa Fisi Kata ya Majengo Manispaa ya Mpanda
Mziray alidai kuwa watuhimiwa hao siku hiyo ya tukio walikamatwa na vipande vinne vya meno ya Tembo vyenye thamani ya shilingi milioni 48 ambapo meno hayo ni sawa na Tembo wawili.
Katika utetezi wake mshitakiwa Godfrey Mabuga aliiomba Mahakama imwachie huru kwa kile achodai kuwa hakutenda kosa hilo bali alisingiziwa tuu na askari waliomkamata wa TANAPA na Polisi .
Mshitakiwa Rashid Ramadhani katika utetezli wake alidai kuwa siku hiyo ya tukio yeye hakuwa mjini Mpanda siku hiyo bali alikuwa Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilayani Mlele hata hivyo alipotakiwa kuonyesha Tiketi ya Basi aliyosafiria alishindwa kuionyesha Mahakamani hapo kama sehemu ya ushahidi wake .
Kabla ya kusoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Chiganga Ntengwa aliiambia Mahakama kutokana na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo washitakiwa Godfrey Mabuga ambae alikuwa ndio mshitakiwa wa kwanza na Rashid Ramadhani ambae alikuwa ni mshitakiwa watatu Mahakama imewatia hatiani baada ya kupatikana na kosa la kifungu cha sheria Namba 86 kidogo cha kwanza na cha pili ya uhifadhi wa wanyama pori Namba 5 ya mwaka 2009 na kfungu cha sheria No57 kidogo cha kwanza sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 marejeo ya mwaka 2000.
Alieleza hata hivyo Mahakama hiyo imemwachia huru mshitakiwa wa pili baada ya kutokuwepo ushahidi wa kumtia hatiani kitendo cha Hakimu kutamka kumwachia huru mshitakiwa watatu washitakiwa hao waliangua kilio Mahakamani hapo huku mshitakiwa wa pili aliachiwa akipiga ishara ya msalaba .
Kisha Hakimu Chiganga Ntengwa alitowa nafasi kwa washitakiwa kama wanayosababu yoyote ya msingi ya kuishawishi Mahakama iliiwapunguzie adhabu hata hivyo washitakiwa hao walidai kuwa hata wakisema wajitetea wanajua adhabu yao haita pungua kikubwa wanachoomba ni kupatiwa nakala ya hukumu yao .
Baada ya hapo mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi Jamira Mziray aliiomba Mahakama itowe adhabu kali kwa washitakiwa kwani kitendo cha kuuwa Tembo kinasababisha wanyama kupungua na kupunguza utalii katika Nchi .
Hakimu Chiganga baada ya kusikiliza pande mbili hizo alisoma hukumu kwa kuiambia Mahakama kuwa washitakiwa hao wote wawili Mahakama imewahukumu kila mmoja kutumikia kifungo cha miaka 20 jela kuanzia juzi .
0 comments:
Post a Comment