Home » » NEWS: WANAFUNZI 15 WA SEKONDARI YA USEVYA WASIMAMISHWA SHULE KWA KOSA LA KUMPIGA MKUU WAO WA SHULE MSAIDIZI NA KUMTOA MENO MATANO

NEWS: WANAFUNZI 15 WA SEKONDARI YA USEVYA WASIMAMISHWA SHULE KWA KOSA LA KUMPIGA MKUU WAO WA SHULE MSAIDIZI NA KUMTOA MENO MATANO


  Na  Walter   Mguluchuma .
       Katavi yetu blog
  Bodi ya   shule ya  Sekondari ya   Usevya   Wilaya  ya  Mlele   Mkoani   Katavi  imewafukuza   shule    wanafunzi   15 wa  Kidato cha Sita wanaodaiwa kuwapiga  walimu wao wawili  kwa kuwachalaza  viboko na kuwashambulia kwa silaha za  jadi  huku  mkuu wao wa  shule  msaidizi kujeruhiwa  vibaya kwenye  sehemu zake za  mwili  na   kung-olewa   meno yake  matano ya  mbele .
  Kikao  cha  Bodi  hiyo  kilifanyika   mwishoni  mwa   wiki  iliyopita  ikiwa  ni  siku  mbili  baada  ya  gazeti  hilo  kuandika   habari ya  tukio la  wanafunzi  hao   kuwashambulia kwa   silaha  za    jadi  zikiwemo  mawe   rungu  na  fimbo  walimu  hao  wawili .
Tukio  la   wanafunzi hao wa  Sekondari   ya  Usevya  kuwapiga  walimu  wao   lilitokea  hapo  Agosti  12   mwaka huu  ambapo  walimu  wawili  walijeruhiwa  vibaya  akiwemo   Mwalimu  Mkuu   Msaidizi  wa  shule  hiyo   Makonda  Ng-oka   ambae  aling-olewa   meno  yake  matano  na  jujeruhiwa  vibaya   kichwani na  mkononi . 
Inadaiwa   chanzo   cha  tukio  hilo   ni  wanafunzi  wa shule  hiyo wa   kidato  cha  sita   shuleni  hapo   kutomtaka   Mwalimu  Ng-oka  kuendelea  kufundisha   kwa  madai   ana  tabia ya  kuwadhalilisha  wanafunzi wa kiume .
Ilielzwa  kuwa  katika   mkasa  huo wa  kupigwa  kwa  walimu hao   siku  hiyo ya  tukio   Mwalimu  huyo   alikuwa  nyumbani  kwake  na  familia   yake  pamoja  na   mgeni   aliyemtembelea   ambae ni  Mwalimu   mwenzake   aitwaye  Gabriel  Kambona .
Ghafla  waliingia   Wanafunzi  kundi  la  Wanafunzi  wakiwa   na  silaha   za   jadi  kama  fimbo  ,marungu  na  matofali   na  kuishambulia  familia  hiyo   muda  huo  Mwalimu   Ng-aka alikuwa  bafuni   anaoga   alisikia   mayowe  ya  familia  yake wakiomba  msaada    alipotoka   aliwakuta  ni wanafunzi  wake  wanawashambulia  kwa  silaha  za  jadi  walipomwona  walimgeukia  na  kuanza  kumpiga   hadi  kupoteza  fahamu .
Katika  kikao  hicho  cha    bodi  kilichokaa  mwishoni  mwa   wiki  iliyopita   bodi  hiyo  imetowa    adhabu    adhabu ya  kuwafukuza  shuleni  hapo  Wanafunzi  hao  15  wa  kidato  cha  sita  kwa  kipindi  cha  wiki  mbili  wasionekane  kwenye  eneo  hilo.
Pia   wanafunzi  hao   kila   mmoja   amepewa  adhabu ya  kulipa  faini  yashilingi   elfu   ishirini  kila  mmoja   na  wanatakiwa  waziwasilishe  pindi  wanapokuwa  kuwa  wamemaliza   adhabu  yao  ya    kutofika  shuleni  hapo .
  Afisa   Elimu  wa  Mkoa  wa  Katavi    Enersti  Hinju   amekili   kufanyika  kwa kikao   cha  bodi ya   shule  hiyo  hapo   Septemba  16  na   taarifa  za uamuzi  wa  kikao   cha  bodi  hiyo  tayari  zipo   osifini  kwake .
Alisema  taarifa  rasmi  za  maamuzi ya kikao  hicho  cha  bodi ya  shule  ataitowa  hivi  karibuni   maana   alikuwa  nje   ya   Mkoa    kikazi  ameripoti  jana   Ofisini  kwake .
Nae   Mwalimu  Gabriel   Kambana  ambae  ni  miongoni mwa   Walimu  walipigwa  na  kutolewa  ngwee  kichwani   alisema  yeye   binafsi   aridhiki  ana   adhabu  hiyo  waliopewa   wanafunzi  hao  kwani  ni  ndogo  hailingani  na  kosa  walilo fanya .
   Alisema   leo hii  wanafunzi  wanawapiga  walimu  wanapewa   adhabu  ndogo  kama  hiyo  jee  siku  mwanafunzi  atakapomgomea  mwalimu   atapewa  adhabu  gani   alihoji  mwalimu  Kambona .
  Alieleza  wao   kama   Walimu wa  shule  hiyo  baada  ya   wiki    moja  baada  ya  kutokea  kwa  tukio  hilo  walikaa  kikao  na  kupendekeza  kuwa    wanafunzi  15  ambao  walikuwa   ndio  viongozi  wa   vurugu  hizo  za    kuwashambulia  Walimu  wafukuzwe  shule  moja  kwa  moja  na  wanafunzi  wengine  zaidi ya  200  wanarudishwe  makwao na  lilikundi  la  tatu  na  wanafunzi  ambao  hawakuwa  kwenye   eneo la  shule  ndio  wabaki  shule  waendelee  na  masomo .
   Kambona  alisema   mapendekezo  hayo   yalipingwa  na   uongozi wa  Halmashauri  yao ya  Mpimbwe  pamoja  na  uongozi  wa  Wilaya ya  Mlele   kwa  kile  walichodai  hawana  mamlaka  hayo  wakati  wao  walimu  wanayomamlaka  ya  kumsimamisha  mwanafunzi  masomo kwa  kipindi  cha      siku  21.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa