Home » » MAHAKAMA ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi imewahukumu watu watatu kutumikia kifungo cha miaka 90 jela baada kupatikana na hatia ya unyang’anyi wa kutumia silaha

MAHAKAMA ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi imewahukumu watu watatu kutumikia kifungo cha miaka 90 jela baada kupatikana na hatia ya unyang’anyi wa kutumia silaha

 
Walter Mguluchuma , Katavi

MAHAKAMA ya Wilaya ya Mlele  mkoani Katavi  imewahukumu  watu watatu
kutumikia  kifungo cha miaka 90 jela  baada  kupatikana na hatia  ya
unyang’anyi wa kutumia silaha na kupora  zaidi ya Sh  milioni 6 –

Washtakiwa hao  ni pamoja  na Shaban Hamis (35)  mkazi wa kijiji cha
Ilunde  wilayani Mlele , Masoud Ramadhani (33)  mkazi wa kijiji  cha
Inyonga  wilayani Mlele  na Ramadhani Agustino (22) mkazi  wa kijiji
cha Kitunda  mkoani Tabora ,  ambapo  kila mmoja  atatumikia  miaka 30
jela .


“Nimetoa  adhabu kali  kwa washtakiwa  ili  iwe  fundisho si  kwako
tu pia kwa wengine  wenye  tabia kama hiyo …. Kosa la unyang’anyi  kwa
 kutumia silaha  adhabu yake  ni kifungo cha miaka 30 jela  kwa kila
mshtakiwa “ alisema Swai .

Mwendesha Mashtka Mkaguzi  wa Polisi , Baraka Hongoli alidai  kuwa
washtakiwa  hao  kwa pamoja walitenda kosa hilo Agosti  21  mwaka huu
saa  nane  usiku katika Mtaa  wa  Uzenga mjini Inyonga ,   wilayani
Mlele .

Ilidaiwa kuwa usiku huo wa tukio  washtakiwa hao  wakiwa na silaha
nzito  aina ya AK 47  walivamia duka la  mfanyabiashara , Jonas Davis
katika Mtaa wa Uzenga   na kumpora zaidi ya Sh  milioni 6.0-

Mwendesha Mashtaka  aliongeza  kuwa  washtakiwa hao  walikamatwa
Septemba 16 , mwaka huu  wakiwa  katika  nyumba ya wageni  Mtaa wa
Isengo  mjini Inyonga, wilayani Mlele  wakijiandaa  kuwapora fedha
wakulima  wa tumbaku .

Ilidaiwa kuwa  baada  ya kukamatwa  na kuhojiwa  walikiri  kwa
maandishi  kuwa  walihusika  na   uporaji  wa  sh milioni 6.0-  na
wakaongoza  askari  polisi  hadi kijijini Ilunde  na  kuonesha
walikoificha  silaha  nzito  aina ya AK 47.

Washtakiwa  hao  watatu wanakabiliwa na mashtak mwengine ambapo
wanashtakiwa  kwa kosa la  kuvamia nyumba ya mkazi  wa kijiji cha
Kalonvya  wilayani Mlele , Patrick Nchimbi  na kumpora  fedha taslimu
, vitu vya thamani  zikiwemo vocha za muda  wa hewani ,  vitenge na
simu za mkononi kwa pamoj vikiwa na thamani  ya Sh  milioni 3.1 .

Pia wanashtakiwa kwa kumjeruhi  kwa  kumpiga risasi  mkononi  mke wa
mfanyabiashara Nchimbi ambapo  mshtakiwa  Shaban Hamis  akikabiliwa
na kesi nyingine  ya  kukutwa na bunduki  iliyotengenezwa kienyeji
‘gobole’ na mtutu  wa bunduki. .

Hakimu  Mfawidhi wa Mahakama hiyo , Swai  amehahirisha keso  zote
mbili   hilo  hadi  Oktoba 12 mwaka  huu zitakapotajwa   tena
mahakamani hapo  baada ya washtakiwa  hao  kukana mashtaka  yao .
Mwisho.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa