Home » » HOT: MKUU WA SHULE MSAIDIZI WA SHULE YA SEKONDARI YA USEVYA MWL. MAKONDA ADAIWA KUPIGWA,KUUMIZWA NA KUTOLEWA MENO MATANO NA WANAFUNZI WA SHULE HIYO.

HOT: MKUU WA SHULE MSAIDIZI WA SHULE YA SEKONDARI YA USEVYA MWL. MAKONDA ADAIWA KUPIGWA,KUUMIZWA NA KUTOLEWA MENO MATANO NA WANAFUNZI WA SHULE HIYO.


Na  Walter  Mguluchuma , Katavi yetu Blog

WANAFUNZI  wa Kidato  cha Sita Shule ya Sekondari Usevya , Halamshauri
  ya Mpimbwe  wilayani Mlele  katika mkoa wa Katavi  wanadaiwa
kuwashambulia  kwa kuwacharaza  viboko  walimu wao wawili  miongoni
mwao akiwa Makamu Mkuu  wa Shule hiyo , Makonda Ng’oka “Membele
‘(34)ambaye amengolewa meno  yake matano .

Inadaiwa kuwa  wanafunzi wa kidato  cha sita shuleni  hapo  hawamtaki
Makamu Mkuu wa Shule hiyo  kuendelea  kufundisha  shuleni  hapo
kutokana kile  wanacho  dai  kuwa   na tabia yake  ya kuwadhalilisha  wanafunzi  wa kiume
shuleni  hapo.

Mwezi  Mei mwaka huu  Ng’oka “Membele” amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya  Mpanda  kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wake kidaiwa kutenda

kosa hilo kati  ya Novemba  2015 na April mwaka huu

Inadaiwa kuwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Makamu Mkuu huyo
wa shule hiyo kulifuatia wanafunzi wa kiume wanaosoma Kidato cha Tano
sasa  wako Kidato cha Sita  katika shule hiyo kumkataa na kutishia
kuandamana kupinga vitendo vyake vya kuwalawiti wanafunzi wake.

Wanafunzi hao walidai kuwa mwalimu huyo amekuwa akiwalawiti baadhi yao
ikiwa ni adhabu mbadala wanapobainika kufanya makosa shuleni hapo.

 Hata  hivyo  baada  ya  kutopatikana  ushahidi wa  kumtia  hatiani
Mwalimu  Makonda  ambapo Julai 27 mwaka huu    Mahakama  ya  Hakimu
Mkazi ya  Wilaya  ya   Mpanda   ilimwachia  huru .

Inadaiwa kuwa  baada  ya mahakama  hiyo kumwachia huru  Mwalimu
Makonda aliripoti  kwenye  kituo chake  cha kazi   , Shule ya
Sekondari  Usevya , Agosti Mosi  mwaka  huu  ambapo  kurejea kwake
shuleni hapo  kunadaiwa kuamsha  hasira kwa wanafunzi  wa Kidato cha
Sita  wakidai  hawapo  tayari  kumwona  mwalimu  huyo  na familia yake
shuleni hapo .

Akiongea  na wanahabari jana  mjini hapa Ng’oka  alidai  kuwa   hayuko
 tayari  kuendelea  kufundisha  kwenye  shule  hiyo kwa kuhofia
usalama  wake  kutoka  na  kipigo  alichokipata  cha  kushambuliwa  na
 baadhi ya  wanafunzi wake wa kidato cha  tano na  cha  sita  wakati
akiwa  nyumbani kwake  na  familia  yake .

 Akisimulia  mkasa  huo  alisema   siku  hiyo ya  tukio , Agosti 12
mwaka  huu  alikuwa   nyumbani  kwake  shuleni hapo  pamoja  na
familia  yake  pamoja  na   mwalimu  mwenzake  aitwae,    Gabriel
Kambona  aliyekuwa  amemtembelea ..

“   Ghafla,  saa  mbili  usiku  nikiwa maliwatoni  nikioga  lilitokea
kundi la  wanafunzi wa kidato cha tano na sita  wakiwa  na  silaha za
jadi  kama vile  fimbo  , malungu , mawe  na  matofali na kuanza
kuishambulia  familia  yake  pamoja  na  mwalimu  Kambona” alieleza

Alidai kuwa alilazimika ‘kuchomoka’ bafuni  baada  ya kusikia mayowe
yaliyokuwa yakipigwa na familia yake  wakiomba msaada  ambapo
alipofika  sebuleni alishuhudia   wanafunzi hao wakiishamulia familia
yake .

“Ndipo walinigeukia  na kuanza kunishamubulia  kwa kunipiga kwa
marungu na fimbo  hadi nikapoteza fahamu  nilizinduka nikiwa
nimelazwa kwenye Kituo cha Afya Usevya  na kubaini kuwa  nimepoteza
meno yangu  matano  huku  nikiwa nimejeruhiwa  kichwani ….

. baadae  nilihamishiwa  katika Hospitali  ya Wilaya  ya Mpanda
ambako  nililazwa wiki moja  na nusu  kwa  matibabu  na sasa nimepewa
rufaa  niende Hospitali ya Taifa  Muhimbili  Jijini Dar  kwa  matibabu
zaidi” alieleza

  Alidai kuwa  uhasama  baina  yake  na   wanafunzi  hao  umedumu kwa
muda mrefu  lakini anashangaa  uongozi wa  Halmashauri  ya  Mpimbwe
na  Wilaya  ya  Mlele  umeshindwa   kumpangia  kituo  kingine  cha
kazi .

“Isitoshe  uongozi wa  Halmashauri ya  Mpimbwe  na  wa wilaya  ya
Mlele  haujawachukulia  hatu yeyote   wanafunzi hao  licha ya
kupeleka majina yao  kwa kuwa nawafahamu  wote  waliohusika  katika
tukio hilo ….. nawafahamu  wanafunzi wake wa kidato cha  sita  ila
wale  wa  kidato cha  tano sikuweza kuwatambua  kwa kuwa  wamejiunga
na  shule  hii  hivi  karibuni …..

Ukweli  ni  kwamba  sikotayari kabisa  i  kukanyaga  tena  kwenye
shule  hiyo  kwani maisha yangu  yako  hatarini  hivyo  naomba
nitafutiwe   shule  nyingine  ya  kufundisha  na  ikiwezekana     iwe
nje  ya  mkoa  Katavi ‘alisisitiza .

  Kabla ya  tukio  hilo  Mwalimu   Makonda   Ng-oga  alifikishwa  katika

Mahakama  ya   Wilaya  ya  Mpanda    hapo   Aprlii  28  mwaka huu  na
kusomewa  mashitaka  ya  tuhuma    za  kulawiti  mwanafunzi  wake  wa
kiume  wa kidato cha  sita  kwa  vipindi  tofauti  vya  kuanzia
Novemba  mwaka  jana  hadi  Aprii     mwaka huu.

Nae  Mwalimu    Gabriel  Kambona   alidai  kuwa  yeye  hayuko  tayari
kuendelea   kufundisha  kwenye  shule  hiyo kwamba kitendo cha kupigwa
 na  wanafunzi wake  kimemfedhesha .

.Kwa mujibu  wa mwalimu  huyo walimu wa shule hiyo waliketi  baada ya
kutokea kwa tukio  hilo ambapo  walifikia maamuzi  kuwa wanafunzi wote
 waliobinika  kushiriki  kuwashamulia walimu wao  wasimamishe  shule
akidai  kuwa  uongozi  wa Halmashauri ya  Mpimbwe  na wilaya ya Mlele
ulipiga .

“Nimesikitishwa  sana na   majibu  yaliyotolewa na  viongozi wa
wilaya  ya Mlele    walipohoji  nimejiingizaje  mpaka  nikapingwa  na
wanafunzi   kama alivyopigwa    mwalimu  Makonda  majibu haya
nidhahri kuwa  wanalidhika  na sisi  kupigwa na  wanafunzi wetu …..

Nimeandika  barua  ya  kuomba  uhamisho   kwani   nia  aibu  kwangu
kuendelea   kufundisha  wanafunzi   ambao  wamenishambukia na  kunitoa
ngeo  kichwani ….. siku  hiyo  ya tukio  niliibiwa simu  mbili za
kiganjani   lakini  jana  nimefanikiwa  kuikamata  simu  moja  kwa
mwanafunzi wa   kidato  cha  tano   anayeitwa ,   Alex  Maiko   Makona
  na   tayari   amemfikisha  katika  Kituo  cha  Polisi  cha  Usevya”
alisisitiza .

Kwa upande wake ,  Mwenyekiti wa   Chama  cha   Walimu (CWT)  Mkoa  wa
 Katavi,  Gregori  Mshota   alikiri kufahamu  mkasa  huo  wa
kushambuliwa  na kujeruhiwa   kwa waili wawili  katika Shule ya
Sekondari  Usevya  ambapo  mmoja wao  alilazwa  katika Hospitali ya
Manispaa  ya Mpanda  kwa  matibabu ..

“ Chama  (CWT)  hicho  tayari  kimeanza   kuwsiliana  na    uongozi
wa   Halmashauri ya  Mpimbwe  na  uongozi  wa  Wilaya  ya   Mlele
ili   kuhakikisha  mwalimu  huyo  anakuwa  salama ……

  Kwa  sasa   jambo hili  halihitaji   mjadala  zaidi  kinachotakiwa
ni  mwalimu  huyo  kupangiwa  kituo  kingine  cha  kazi   ili
kununusuru  uhai  wakwe  uamuzi   huu  ulipaswa  uwe  umefanyika
mapema “ alisisitiza .

Nae  Ofisa  Elimu  wa  Mkoa  wa  Katavi  , Ernesti  Hinju
alipotafutwa  ili  aweze  kuelezea   tatizo  hilo  alisema  yeye  yuko
  nje  ya  mkoa   kikazi   ila  swala  hilo  lipo  katika   ofisi
yake  na  wameisha  anza  kulichakata .

Alisema   swala  hilo  linahitaji  vyombo  mbalimbali   kwa  ajiri ya
kulipatia  ufumbuzi  swala  hilo  ikiwemo  bodi ya  shule ya
Sekondari  ya  Usevya .

Wakati wa  ziara  ya  Waziri  Mkuu   Kassim  Majaliwa  alioifanya
mwezi  uliopita   mke wa  Mwalimu   Makonda  Ng-oga   alikwenda
kwenye  mkutano wa  hadhara  uliofanyika  katika   Kijiji   cha  Maji
Moto  huku  akiwa  na   bango la  lililokuwa  limeandikwa  juu  ya
familia   yake  kutishiwa  amani   hari  ambayo  ilimfanya  Waziri
Mkuu   amwagize    Kamanda  wa  Polisi  wa  Mkoa  wa  Katavi
ashughulikie  swala  la  malalamiko  hayo .

Juhudi za  kumpata   aliyekuwa  mwanafunzi wa  shule  hiyo
aliyemaliza   kidato  cha  sita  mwaka  huu  ambae  anatuhumiwa
kulawitiwa na  mwalimu  huyo aliaweze  kuthibitisha   mahusiano  yake
na  Makonda   azikuweza  kufanikiwa  hakuweza  kupatikana  kwa  njia
ya  simu  huko   aliko    Wilayani   Misungwi.

 Mwisho



0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa