Home » » MAJALIWA -MARUFUKU DC KULIA NJAA KWENYE ENEO LAKE

MAJALIWA -MARUFUKU DC KULIA NJAA KWENYE ENEO LAKE


  Na  Walter  Mguluchuma  .
      Katavi .
  Waziri  Mkuu wa  Serikali ya  Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania  Kassimu  Majaliwa  amewaagiza  wakuu wa  Wilaya  wote  hapa  Nchini  kuhakikisha  watu wote wanao waongoza  wanafanya  kazi na  Serikali   haita  kubali wala  haitaki kusikia  Mkuu wa  Wilaya  analia    njaa kwenye  Wilaya yake ..
  Agizo  hilo  alilitowa  hapo  juzi  wakati  alipokuwa  akiongea  na  watumishi wa  Halmashauri  zote  tano za  Mkoa  wa  Katavi  pamoja  na  viongozi wa  taasisi   mbalimbali na  viongozi wa  dini  katika   Ikulu   ya  Mpanda .
 Alisema  Serikali  haitaki  kusikia  Mkuu wa  Wilaya  analia  njaa  kwenye  Wilaya   yake  kutokana  na  uzembe wa  watu wake  kutofanya  kazi  na kutolima  hivyo   wakuu wa  Wilaya   wanao  wajibu wa kuwasimamia  watu  wao  wafanye  kazi .
 Alisema kila  Mkuu wa  Wilaya  hapa  Nchini   kwenye  Wilaya  yake   ahakikishe anawawahamasisha  wananchi  wake  walime   ili   waweze  kujitoshereza  kwa  chakula  kwenye  maeneo  yao .
 Alisisitiza  kuwa  Serikali itapeleka   msaada wa  chakula  kwenye   Wilaya  ambayo  imepata  upungufu wa  chakula  kutokana  na  sababu   ile  ambayo haizuiliki  kama   vile     hari  ya  ukame na sivinginavyo .
 Alieleza  Serikali  imepanga  na  itahakikisha  pembeo   za  kilimo zinawawafikia  wakulima   kwenye   maeneo  yao  kabla ya  miezi  miwili  ya kuanza kwa msimu  wa kilimo .
Kwa  upande wa watumishi  aliwataka watambue kuwa wao  ni watumishi  wa  Wantania  hivyo wanakiwa  kuwahudumia  watu kwa kuwapokea  na kuwasikiliza na  kuwahudumia .
 Alisema  Serikali ya  awamu ya   tano inasisitiza  uwajibikaji   inataka  watumishi  wote  hapa   nchi      wafanye   kazi  na wabadilike   katika  utendaji wao wa kazi  na kila   mtumishi  anakuwa   mwadilifu .
Majaliwa   alieleza   Serikali   imeongeza    bajeti  ya   fedha  za  maendeleo   kutoka   asilia    27  hadi  kufikia   asilia   40  hivyo   fedha    watumishi wanakiwa  kuwa  waminifu wa  kusimamia  fedha  hizo .
  Hivyo  aliwaka   madiwani  kuhakikisha  wanasimamia   fedha  hizo  kwenye   Halmashauri  zao na  miradi  inayo jengwa inalingana  na   fedha  zilzopokelewa  na  miradi    inajengwa  kwa   ubora  unao  lingana  na   fedha .
  Awali   Mkuu wa  Mkoa  wa  Katavi  wa   Katavi  Meja   Generali  Mstaafu  Raphael   Muhuga   alisoma   taarifa   ya   maendeleo ya   mkoa huo      ambapo   alisema  Mkoa wa   Katavi  umeandaa  mazingira ya  uwekezaji  ili  wananchi wake   waondokane  na  umasikini  ifikiapo  mwaka    2026.
 Alisema  Mkoa  wa   Katavi  unakabiliwa  na baadhi ya   changamoto   mbalimbali  ikiwemo  ya  Mkoa  huo  kutokuwa  na   Hospitali ya  Mkoa  .
Changamoto   nyingine  ni   tatizo  la  umeme     kukatika   mara kwa  mara  kutokana  na   uchakavu wa  jenereta za  mashine   ambazo  kabla ya kuletwa   Mkoani  Katavi mwaka  1993  zilikuwa  zimeisha  tumika Mkoani  Shinyanga kwa  kipindi  cha  miaka   kumi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa