Home » » HOT:MCHUNGAJI WA KANISA LA MOROVIANI JELA MIAKA 20 KWA KOSA LA KUPATIKANA NA MENO YA TEMBO YA TSH MILIONI 90 YAKIWA NDANI YA KANISA

HOT:MCHUNGAJI WA KANISA LA MOROVIANI JELA MIAKA 20 KWA KOSA LA KUPATIKANA NA MENO YA TEMBO YA TSH MILIONI 90 YAKIWA NDANI YA KANISA

 
Na  Walter   Mguluchuma .
                        Katavi
  Mahakama ya  Wilaya ya  Mpanda  Mkoa wa  Katavi  imemuhukumu   Mchungaji wa Kanisa la Moroviani  Usevya Wilaya ya Mlele  Mkoani  hapa Godwel Siame  kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana  na  hatia ya kukamatwa na  nyara za Serikali  meno ya  Tembo yenye  thamani ya Tsh Milioni 90 akiwa  ameyahifadhi  ndani ya  Kanisa .
Hukumu  hiyo   ilivutia hisia za  watu  wengi wa Manispaa  ya  Mpanda  na  Mkoa wa  Katavi   ilitolewa  hapo  jana  na Hakimu  Mkazi   Mfawidhi wa  Mahakama ya  Wilaya ya  Mpanda  Chiganga  Ntengwa  baada ya Mahakama  kuridhika   na  ushahidi  uliotolewa  Mahakamani  hapo na   upende wa  mashitaka na utetezi .
Katika   kesi  hiyo   upande wa  mashitaka uliongozwa na Mwanasheria mfawidhi wa  Serikali wa  Mkoa wa  Katavi   Acheres  Mliso na  mshitakiwa  Mchungaji  Siame  alitetewa na wakili  Patrick  Mwakyusa  ambapo  upande wa  mashitaka ulikuwa na  mashahidi sita  na  upande wa utetezi ulikuwa na  mashahidi wane .
Awali  katika  kesi  hiyo  mwendesha  mashitaka wa  Serikali  Acheres  Mliso  alidai kuwa   mshitakiwa   Mchungaji   Godwel  Siame  alitenda kosa  hilo  hapo  Mei   5 mwaka  huu katika Kijiji  cha  Usevya  Wilaya ya  Mlele .
Siku  hiyo ya  tukio  mshitakiwa  ambae  alikuwa ni  mchungaji wa  Kanisa  la  Moroviani  Usevya  alikamatwa na  Askari wa  Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi na  Askari wa  jeshi la  Polisi   akiwa na  Nyara za  Serikali  Meno ya  Tembo vipande 11  vyevye uzito wa kilo 20 yenye  thamani ya Tsh  Milioni  90  akiwa  ameyahifadhi  ndani ya  Kanisa la  Moroviani  Usevya  alikuwa  akiliongoza  kama  mchungaji wa  Kanisa  hilo.
 Ilidaiwa  kuwa  aSkari wa  Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi  pamoja  na  Askari  Polisi walipata  taarifa   kutoka kwa  Raia  wema wa  Kijiji  cha  Usevya kuwa   mchungaji  Godwel  Siame  anajishughulisha  na  biashara ya  meno ya  Tembo   na  amekuwa  akiyahifadhi  ndani ya  Kanisa  analoliongoza .
Mwendesha   mashitaka  huyo wa   Serikali  alidai  kuwa    baada ya  taarifa  hizo  polisi  na  Askari Tanapa walifika  katika   eneo hilo  siku hiyo na  ndipo walipoweza  kufanikiwa   kukamata   meno  yaTembo   vipande  11  yenye  thamani ya Tsh Milioni  90 yakiwa yamehifadhiwa  ndani ya  Kanisa  Moroviani  Usevya.
Hakimu  Mkazi   Mfawidhi Chiganga  Ntengwa  kabla ya kusoma  hukumu aliiambia  Mahakama  kuwa  kutoka  na  ushahidi  uliotolewa   Mahakamani  hapo wa  pande  zote mbili za  mashitaka na  utetezi  Mahakama  pasipo  shaka  yoyote  imeona  mshitakiwa   anayo  hatia  hivyo kw  misingi  hiyo inampa  nafasi mshitakiwa  kama  anayosababu yoyote ya  msingi ya kuishawishi  Mahakama  impunguzie  adhabu .
Katika   utetezi wake  mchungaji  Siame  aliliomba  Mahakama  imwachie  huru  kwani  yeye hakujua   kama  ndani ya   Kanisa  lake  kuna  Meno ya  Tembo  yamehifadhiwa  humo   na  ndio  maana walipomkamata   wakati akiwa  nyumbani  kwake  hakuwa  na   shaka  yoyote  ile .
 Utetezi huo ulipingwa  vikali na   Mwendesha  Mashitaka  Mwanashria   Mfawidhi wa  Serikali  wa   Mkoa wa  Katavi   Acheres  Mliso   ambae  aliiomba   Mahakama  ipatie   adhabu  kali  mshitakiwa  ili iwe  fundisho kwa viongozi  wenzake wa  Dini  ambao  wanatabia  kama  hiyo .
 Hakimu  Chiganga baada ya  kusikia  maombi ya  mshitakiwa  aliiambia  Mahakama kuwa  mshitakiwa  Mchungaji   Godwel Siame amapatikana  na  hatia  ya kifungu cha    sheria  N0  86  kifungu kidogo cha kwanza na cha pili  cha  sheria  ya  uhifadhi wa  wanyama  pori  N0  5 ya mwaka   2009 na  kifungu cha  sheria   N0 57 kifungu kidogo cha kwanza  cha  sheria ya uhujumu  uchumi  sura   N0 200  marejeo ya mwka 2000.
 Hivyo  Mahakama  imemuhukumu  Mchungaji  Godwel  Siame  kutumikia  kifungo cha   miaka  ishirini  jela  kuanzia  jana  na    kama  haja  ridhika na  uamuzi huo  unaruhusiwa kuomba  rufaa  ndani ya siku  30  kuanzia  jana

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa