Home » » HOT NEWS: VIONGOZI WA CCM MKOA WA KATAVI WAGAWANYIKA NA KUGAWANA OFISI

HOT NEWS: VIONGOZI WA CCM MKOA WA KATAVI WAGAWANYIKA NA KUGAWANA OFISI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


     Na  Walter  Mguluchuma  Na  Irine  Temu
         Katavi  Yetu blog
  Mgwawanyiko  mkubwa  umetokea   ndani ya  viongozi wa  ngazi za juu wa  Chama   cha  Mapinduzi  CCM  Mkoa   wa  Katavi   hari  ambayo  imepelekea  Mwenyekiti  wa  CCM wa  Mkoa    Mselemu  Abdala  na  Katibu wa  wake  Everni  Mushi  kugawana   ofisi  katika  maeneo  tofauti huku  Katibu wa  CCM akiwa  amehamishia  ofisi yake  katika   chumba  kilichokuwa kikitumiwa  na  bendi ya  muziki ya  Mpanda  jazz .
Mgawawanyiko huo  pia  umesababisha  kuwepo kwa  makundi  mawili   ndani ya  viongozi  hao wa  ngazi ya juu  ambapo   kundi  moja  linalomuunga  mkono  mwenyekiti  huyo  ni la baadhi  ya  wajumbe wa  kamati ya  siasa  ya Mkoa  na  Katibu   anaungwa  mkono  na  Sektarieti ya Mkoa  huo .
Mmoja   wa  viongozi  wa   Chama  hicho  wa  ngazi ya  Mkoa ya  Mkoa  ambae  akutaka jina  lake  litajwe  aliwaambia  waandishi wa   Habari  jana  kuwa   kutokana  na  mgawanyiko  baina ya  viongozi  hao  wawili  wa  ngazi  ya juu wa Mkoa  huu  umesababisha  viongoozi  hao  watengane  kwa  kugawana   ofisi  katika  maeneo  mawili  tofauti  aliyoko  katika  Mji wa Mpanda .
 Alisema  Mwenyekiti  wa  CCM   yeye   pamoja  na  baadhi ya  wajumbe  wa  kamati ya  siasa  wa  Mkoa  wamekuwa  wakifanyia  shughuli  zao   katika  jingo  linaloendelea  kujengwa lililopo  katika   Maeneo ya  Mtaa wa  Majengo  jirani na  Posta  na  katibu  wa  CCM  na  Katibu  wa   Vijana na  mchumi wa  Mkoa wamehamia   katika  jingo la  ofisi ya   CCM  wilaya  ya   Mpanda .
 Kiongozi  huyo  alieleza  kuwa    viongozi  hao  wamekuwa  na  mvutano kwa  kipindi  cha  zaidi ya  miezi mine  sasa  huku    mwenyekiti  wa   chama  hicho  akitataka  ofisi  yao  ihamishwe  kutoka   Katika   Mtaa wa  Ilembo walikokuwa  wamepanga  baada ya  muda wao  kuwa  umekwisha  na  wahamie  katika   katika  jingo  lao  ambalo  linaendelea  kujengwa  .
  Huku  Mushi   akiwa yeye  anataka   ofisi  zao  zihamie  kwenye  jingo  la  ofisi ya     ccm  Wilaya ya  Mpanda  hadi  hapo   jingo  lao la  ofisi    litakapo  kuwa  limekamilika .
 Alisema  hivi  karibuni   Mwenyekiti  wa    CCM  Mselemu  Abdala   aliamuru  ofisi  hiyo  ihamie  kwenye  jingo lao   linaloendelea  kujengwa  na  wakati  huo  Mushi  akiwa   safarini   hari  ambayo ilipelekea  Katibu  wa Vijana   aliyekuwa  anakaimu  nafasi ya   Katibu  wa  Mkoa  kutokubaliana  na  maagizo  hayo kwa  kile alichodai  hawezi  kuhamisha  ofisi  wakati   Katibu  wa  Mkoa   ayupo.
Hari  hiyo  ilimfanya   mwenyekiti wa  CCM  wa  Mkoa   aongozane  na   wajumbe  wawili wa   Kamati ya  siasa ya  Mkoa  ambao pia  ni   madiwani wa  Kata  ya   Kasokola  na   Mpandahotel  pampja  na  katibu wa  jumuia  ya  wazazi wa  Mkoa  na  kuhamisha  ofisi ya Mwenyekiti na  kuhamishia   kwenye  jingo  lao katika  Mtaa wa  Majengo .
Baada  ya  Mushi  kurejea    Mjini   Mpanda   hapo  juzi  na kukuta   Mwenyekiti  wake amehamisha  ofisi  yake  nae  aliamua  hapo  jana   kuhamishia ofisi  yake katika    chumba  kilichokuwa  kinatumiwa  na  bendi ya  muziki ya  Mpanda  jazz   katika  jingo  la  Ofisi ya  CCM  Wilaya  ya  Mpanda  huku  akiwa   anadai   kuwa  hawezi  kuhamia  kwenye  jingo la  ofisi  ambalo  mwenyekiti wake  anataka  wahamie wakati likiwa  halina  wala  sakafu  chini  na  milingo  halina wala dali.
Mwenyekiti  wa  CCM  wa  Wilaya  ya  Mpanda  Beda   Katani   amelisema  kuwa  ametapa  taarifa   za  kuhamia   kwenye  ofisi  ya  CCM  kwa  Katibu  wa  Mkoa   kwenye  jingo la Ofisi  za  Wilaya .
  Alisema ingawa  emehamia  kwenye  jingo  hilo la  Wilaya  yeye  kama  mwenyekiti  hakuwa  amepata  ombi lolote  kutoka kwa  Katibu  huyo wa  Mkoa .
Beda  alieleza  kuwa  baadhi ya  vifaa  alivyohamishia hapo  vimelazika  kuhifadhiwa  katika  ofisi ya    mchumii wa   CCM   wa  Wilaya ya  Mpanda.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa