Home » » NI HATARE HII: MWALIMU MKUU MSAIDIZI WASEKONDARI KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KULAWITI MWANAFUNZI WAKE WA KIDATO CHA TANO WA JINSIA YA KIUME

NI HATARE HII: MWALIMU MKUU MSAIDIZI WASEKONDARI KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KULAWITI MWANAFUNZI WAKE WA KIDATO CHA TANO WA JINSIA YA KIUME

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na  Walter  Mguluchuma 
          Katavi yetu Blog
Mwamlimu  Mkuu msaidizi  wa  shule ya    Sekondari     Usevya  Tarafa  ya  Mpimbwe  Wilaya  ya  Mlele  Mkoa  wa  Katavi   Makonda   Ng-onga  amefikishwa kizimbani  katika  Mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhumma  za  kumlawiti wanafunzi wake wa kiume wa kidato cha tano ambaejina  lakelimehifadhiwa kinyume na maumbile yake .
Mtuhumiwa  alifikishwa kizimbani hapo  juzi  na  kusomewa  mashita  na  mwanasheria wa  Serikali  Mkoa  wa  Katavi   Gregoli   Mhagwa    mbele  ya  Hakimu   Mkazi  mfawidhi wa  Mahakama  ya  Mpanda  Chiganga  Ntengwa .
Mwanasheria  huyo wa   Serikali  alidai  kuwa  mtuhumiwa  anadaiwa  kutenda  kosa  hilo  hapo    Novemba   mwaka  jana   hadi    Aprili  mwaka  huu kwa  nyakati  tofauti  huko  katika   eneo  la  shule  ya  Sekondari ya Usevya   Tarafa  ya   Mpimbwe  Wilayani  Mlele .
Gregoi l aliiakuiambia   mahakama  kuwa   mtuhumiwa  alitenda kosa  hilo la kumwingilia   kinyume  na  maumbile  yake ya kiume mwanafunzi wake wa  kidato cha  tano wa shule  hiyo  kwa kutumia  nafasi yake ya mkuu wa  shule  msaidizi .
 Alisema   Makonda  anashitakiwa kwa kosa  la kifungu  cha  sheria   Namba    154 kifungu  kidogo a  sura  ya  16 ya  sheria ya  marekebisho ya sheria  ya  mwaka  2002.
 Mtuhumiwa anadaiwa kutenda  kosa  hilo  baada  ya  kuwa mwanafunzi huyo anapokuwa  amefanya  kosa shuleni   hivyo  hulazimisha kumwingila  kinyume cha maumbile yake   vinginevyo  kama  mwanafunzi  huyo  atakataa amekuwa akimtishia   kumfukuza  shule .
Mwanasheria  wa  Serikali  baada ya kusomea  mashita  hayo  mthumiwa  Makonda  alikana  kutenda  kosa  hilo   mbele  ya Hakimu   Mkazi  mfawidhi   wa  Mahakama  hiyo  Chiganga  Ntengwa .
  Hakimu  Chiganga   aliharisha  kesi  hiyo  hadi  hapo  june  27 itakapotanjwa  tena  na  mshitakiwa  aliweza  kupata  mdhamana  baada ya  kutimiza  masharti ya  amdhamana  ambapo  alitakiwa  kuwa  na  mdhamini  mmoja  ambae  alisaini  hati  ya  shilingi  milioni  tatu  mahakamani hapo .
 Kablayatukio  hilo  la  mtuhumiwa   kufikishwa Mahakamani wanafunzi washule  hiyo walimkaa mwalimu huyo  mbele yaAfisa ElimuwaMkoa   wa  Katavi Eneresti Hinju kwa  kile walichodai kuwa amekuwa akiwafanyia vitendo vya  kuwalawiti baadhi ya wanafunzi wavulana  wanaosoma katika  Sekondarihiyo ya Usevya.
MWISHO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa