Home » » KUTOKA MPANDA: DC AWATAKA MADADA POA KUFIKA OFISINI KWAKE ILI WAPATIWE ELIMU YA KUUNDA VIKUNDI VYA UJASILIA MALI

KUTOKA MPANDA: DC AWATAKA MADADA POA KUFIKA OFISINI KWAKE ILI WAPATIWE ELIMU YA KUUNDA VIKUNDI VYA UJASILIA MALI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
   
N a  Walter  Mguluchuma 
     Katavi yetu blog
  Mkuu wa  Wilaya  ya  Mpanda   Paza   Mwamlima  amewataka   akinadada   POA  wanauza  miili yao   katika  Mitaa  mbalimbali ya  Manspaa ya   Mpanda  kuacha  tabia ya kuuza miili yao  wafike  ofisini  kwake  ili  awapatie  wataalamu  wa kuwaelimisha kuunda  vikundi  vitakavyo wawezesha  kujiinua kiuchumi badala ya kuuza mili yao .

Kauli  hiyo ya  Mkuu wa  Wilaya ya  Mpanda   ameitowa  ikiwa ni  siku  chache baada ya kuwa  ameliagiza  jeshi la Polisi  Wilayani  Mpanda  kufanya  msako  wa kuwakamata  na kuwaondosha  akina  dada   POA  wote wanaofanya  biashara ya  kuuza miili yao  katika  Mitaa ya  Mji wa  Mpanda .

Mwamlima  aliwaambia waandishi wa  Habari  juzi kuwa  mbali ya  agizo hilo ameliagiza  jeshi hilo kufanya  ukaguzi wa kuzibaini   nyumba  zote  Bubu za  kulala  wageni na  na zitakazobaini wazifunge  mara moja kwani  ndio  ambazo  zimekuwa  zikitumiwa na  akina  Dada   POA  kufanyia biashara ya kuuza mili yao.

 Aliitaja mitaa ambayo hasa  inatakiwa  zoezi  hilo lifanyike  kuwa  ni  M itaa ya  Simba ,  Fisi  na  Mtaa wa  Majengo  ambayo ndio  inayoongoza kwa biashara ya  Dada  poa .

 Alisema  kuliko wao  akina  Dada wanao uza  miili  yao  kuendelea kukamatwa  kamatwa  waambieni waje  ofisini  ili awapatie wataalamu  watakao waelekeza  namna ya kuunda vikundi  vitakavyo wasaidia  kukopesheka na  kuweza kuwainua kiuchumi na kuwafanya wajitegemee.

  Hivi  karibuni  biashara ya  akina  Dada  wanaouza miili yao imeshamili  sana  katika  Mji wa Mpanda baada ya  kuvamiwa  na   akina  dada  poa  ambao  wengi wao wametoka   katika  Mikoa ya  Mwanza  Shinyanga ,  Mbeya na  Kigoma.

Na wamekuwa wakimiliki nyumba  mbili za kulala wageni  katika  Mta a wa Majengo  B  baada ya kudai  kuwa  kwenye  madanguro wamekuwa wakisuburiwa kwa kukamatwa mara kwa mara  tofauti na walivyo  hamia   kwenye  Geusti hizo wamekuwa  awasumbuliwi kwa kuwa wanachangia kodi ya  Serikali kutokana  na  malipo wanayo  mlipa  mwenye  Geusti  alisema  Dada  Poa aliyejitambulisha kwa jina la  Eliza   mwenyeji wa Mwanza  alipokuwa akionge na  gazeti hili  katika  Mtaa wa Fisi.

 Alisema wateja wao  wanaowapa  kwa  wingi  ni  vijana   mwenye  umri  unaoanzia   miaka   16 na  baadhi yao ni  wanafunzi wavulana wa shule za Sekondari  na  biashara  hiyo ya kuuza  miili yao huwa wanaanzia shilingi  2,000 na kwasiku  moja  huwa wanapata  kiasi kisichopungua shilingi  15,000 kwa siku .

Mmoja wa  wakazi  anae  ishi  kwenye  mtaa huo  Osca  Selemani  alieleza kuwa  foleni ya wanaume  wanaowafuata  akina  dada  Poa huwa  inaanza kuanzia saa moja  na  nusu  jioni   hadi saa sita usiku   ndipo wakundi  hayo ya  wanaume yanapopungua .

Alisema  yeye  binafsi  anajuta  kujenga  nyumba  na kuishi   kwenye  mtaa huo kutokana  na  mtaa huo kuonekana kuwa  hauna  heshima  kwenye  jamii hali  ambayo inamfanya ikifikia  mida ya jioni  kwenda yeye  mwenyewe kutafuta  mahitaji dukani kwa kuhofia  mke wake na  mtoto wake wa kike  nao pia wanaweza wakadhaniwa ni  Dada  POA.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa