Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kamanda wa Polisi Mkowa wa Katavi Dhahiri Kidavashari
MWANAFUNZI AFA MAJI MTONI WAKATI AKIWA ANAVUA SAMAKI
Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
Mwanafunzi wa darasa la sita
shule ya Msingi Kashato Manspaa ya Mpanda Julias Justine 12
amekufa maji wakati akiwa anavua
samaki katika mto Mpanda eneo la Kigamboni wakati akiwa na wanafunzi wenzake.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari
aliwaambia jana waandishi wa habari
jana kuwa tukio hilo lilitokea
hapo juzi majira ya saa saa sita mchana
katika mto Mpanda eneo la Kigamboni.
Siku hiyo ya tukio
mama mzazi wa marehemu
anaitwa Prisca Selemani alimwagiza
marehemu dukani kwenda kununua
sabuni ya kufulia nguo baada ya kuwa amemwagiza
yeye alikwenda msibani katika
Mtaa wa Nsemlwa.
Kamanda Kidavashari alieleza
wakati marehemu alipokuwa anakwenda dukani alikutana na watoto wenzake
ambao walimshawishi asiende kununua sabuni na badala yake wakanunue doano ya
kuvulia samaki nae alikubaliana na
watoto wenzake na alinunua doano badala
ya sabuni na kasha walielekea mtoni kuvua samaki.
Mama yake yake alirudi nyumbani muda wa saa 12 jioni kutoka msibani alikokuwa amekwenda na hakuweza
kumkuta nyumbani na alianza
kumkutafuta kwa majirani zake na kuweza kufanikiwa kumpata.
Alisema ndipo hapo
jana walipomweleza kuwa walimwona mwanae akiwa anavua samaki kwenye mto wa Mpanda eneo la Kigamboni huku akiwa na watoto wenzake.
Ndipo jitihada za kumtafuta zilipoanza
za kwenye mto Mpanda na ilipofikia majira ya saa nne asubuhi walipofanikiwa kuupata mwili wa marehemu akiwa ameisha kufa
maji katika mto eneo la Kigamboni.
Kidavashari alisema baada ya mwili wa marehemu kufanyiwa
uchunguzi walikabidhiwa ndugu wa marehemu kwa ajiri ya mazishi ambapo mazishi
yalifanyika katika makaburi ya Shanwe.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi ametowa wito kwa jamii kuwaelimisha watoto kuacha
tabia ya kwenda kucheza ,kuogelea au kuvua samaki kwenye mito na madimbwi hasa wakati huu wa
mvua ili kuweza kujiepusha
na matukio ya namna hii yasijitokeze ndani ya jamii
0 comments:
Post a Comment