Home » » SIMBA AVAMIA KIJIJI NA KUUWA BABA NA MWANAE BABA ANYONYWA DAMU NA SIMBA HADI KUFA MTOTO ALIWA NA KUBAKIA KICHWA TUU‏

SIMBA AVAMIA KIJIJI NA KUUWA BABA NA MWANAE BABA ANYONYWA DAMU NA SIMBA HADI KUFA MTOTO ALIWA NA KUBAKIA KICHWA TUU‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
   Katavi
Mnyama Simba amevamia Kijiji cha Sitalike  Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi na kuuwa watu wawili mtu na mtoto wake kwa  kumla mtoto na kuachi  kichwa na baba yake mzazi  kunyonywa damu na simba huyo hadi kufariki Dunia.
 Tukio la Simba huyo kuuwa watu wawili limetokea hapo hapo jana majira ya saa kumi na moja alifajiri katika Kijiji hicho cha Sitalike .
Mwenyekiti wa Kijiji  hicho Cristophar Anjelo  aliwaambia waandishi wa Habari jana kuwa marehemu  waliouwawa  na Simba  kuwa ni  John Jeremia (45) na  mwanae wa kiume mwenye umri wa miaka mitano .
 Alisema  siku hiyo ya tukio wanafamilia hao walikuwa wamelala ndani ya nyumba yao  ndipo simba huyo jike alipovamia na kuingia ndani ya nyumba hiyo ambayo haikuwa na uwimala  na kuwavaa watu mtu na mtoto wake .
 Alieleza  baada ya Simba huyo kuingia ndani alimvamia  baba wa mtoto huyo na kuanza  kumnyonya damu hadi alipohakikisha amefariki Dunia ndipo alipo mwachia marehemu huyo.
Mwenyekiti huyo wa Kijiji alisema simba  huyo baada ya kuona   John  Jeremia amemnyonya damu hadi kufa alihamia kwa mtoto wake na marehemu na  kuanza kumshambulia na  kisha alianza kumtafuna na  kubakia kichwa   huku mwili wake wote wa mtoto huyo  kuliwa wote.
 Simba  baada ya kuwa amekula mwili wa mtoto alichukua kichwa cha marehemu mtoto na kwenda nacho hadi  kwenye kichaka kilichokuwa jirani na nyumba ya marehemu hao.
 Alisema taarifa za kuuwa na simba kwa marehemu hao zilifika kwenye uongozi wa Kijiji hicho ambao nao walitowa taarifa kwa Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi ambapo walianza kufanya msako wa kumsaka simba huyo kwa kushirikiana na Wananchi wa Kijiji cha Sitalike.
 Wakati walipokuwa wakifanya msako walionanyayo za simba na walizifuata  kule zilipoelekea na walipofika kwenye kichaka walimuona simba huyo akiwa amekaa na pembeni yake  kukiwa na kichwa cha marehemu  mtoto .
Mwenyekiti wa Kijiji alisema Askari wa Hifadhi ya  Katavi walimfyatulia simba huyo risasi lakini aliweza  kuikwepa na kusogea mbele zaidi .
Hata hivyo waliendelea kumfuata  kwa kushirikiana na wananchi ndipo Askari wa TANAPA walipofanikiwa  kupiga risasi na kufa hapo hapo
Alieleza baada ya Simba  huyo kuwa ameuwawa kwa kupigwa risasi baadhi ya wananchi waliomba wamchukue  kama kitoweo cha mboga  lakini Askari wa TANAPA waliwakatalia na walimchukua simba huyo  aliyekuwa amekufa  na kwenda  nae  kwenye hifadhi yao kwa kile walichoeleza kuwa wanakwenda kumchoma moto kwa kutumia mafuta ya petroli.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha kuuwawa kwa watu hao na Simba huyo aliyetokea kwenye Hifadhi ya mbuga ya Katavi .
Alisema  ameisha peleka askari wake kwenda kuangalia  eneo la tukio hilo na ametowa wito kwa wananchi kuacha kujenga makazi karibu na hifadhi ya Katavi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa