Home » » JESHI la polisi mkoa wa Katavi limegoma kuusafirisha mwili wa askari polisi PC H 305 Nobart Chacha(25) ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi kifuani wakati akifanya ujambazi

JESHI la polisi mkoa wa Katavi limegoma kuusafirisha mwili wa askari polisi PC H 305 Nobart Chacha(25) ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi kifuani wakati akifanya ujambazi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Na Walter Mguluchuma   Katavi

. JESHI la polisi mkoa wa Katavi limegoma kuusafirisha mwili wa askari polisi PC H 305 Nobart Chacha(25) ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi kifuani wakati akifanya ujambazi nyumbani kwa mfanyabiashara mmoja wa madini.

Kwa mujibu wa habari zilipatikana kutoka mjini Mpanda, zinaeleza kuwa mwili wa marehermu huyo umesafirishwa jana kuelekea mkoani Mara ambapo baadhi ya marafiki,Chama cha watu wa Mara waishio mkoani Katavi ndio walichukua jukumu la kugharamia usafirishaji wa mwili huo.

MMoja wa wajumbe katika Chama hicho, Julius Marwa alisema kuwa wamelazimika kusafirisha mwili huo wa marehemu baada ya polisi kukataa kuusafirisha kwa madai kwa kitendo alichofanya askari huo tayari amejifukuzisha kazi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema kwamba kwa taratibu za kijeshi mwili wake haustahili pewa heshima yoyote ikiwa pamoja na kusafirishwa kwa kuwa tayari amejifukuzisha kwa aibu na fedhea kubwa kutokana na kitendo alichofanya.

Askari Polisi huyo wa kituo cha polisi wilaya ya Mpanda, aliuawa majuzi nyakati za usiku wakati akiwa katika harakati za kufanya ujambazi nyumbani kwa mfanyabiashara wa madini Daniel John katika Kijiji cha  Ibindi  kilichopo Kata ya Machimboni Wilayani Mlele.

Kwa mujibu wa  Diwani wa Kata ya Machimboni,  Raphael Kalinga, polisi huyo akiwa na kundi la majambazi wenzake ambao idadi yao hakufahamika mara moja walifika kijijini hapo kwa lengo la kumvumia na kumpora kwa kutumia silaha mfanya biashara huyo wa Madini ya dhahabu na mashine za kusaga.


Inadaiwa kuwa, majambazi hao walivunja mlango kuingia ndani ya nyumba hiyo na kumwamuru mfanyabiashara huyo kukaa kimya lakini hakutii agizo hilo ambapo alichukua bunduki yake ya aina ya Shortgun na kufyatua risasi ambayo ilimpiga Askari Polisi huyo katika sehemu ya kifuani na mgongoni na kufa hapo hapo.
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa