Home » » HATARI: ASKARI POLISI MWENYE UMRI WA MIAKA 25 AUAWA KWA KUPIGWA RISASI WAKATI AKITAKA KUFANYA UJAMBAZI

HATARI: ASKARI POLISI MWENYE UMRI WA MIAKA 25 AUAWA KWA KUPIGWA RISASI WAKATI AKITAKA KUFANYA UJAMBAZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu blog
Askari wa Jeshi la Polisi  wa Wilaya ya Mpanda Mkoa Katavi  Pc  H 305  Nobart Chacha(25) ameuwawa kwa kupigwa Risasi kifuani na mgongoni  wakati akiwa  anataka kufanya ujambazi na kupora  mali za mfanyabiashara wa Madini.
Mauwaji ya Askari wa  huyo wa jeshi la Polisi  lilitokea hapo jana muda wa saa nane usiku katika Kijiji cha  Ibindi  Kata ya Machimboni Wilayani Mlele.
 Diwani wa Kata ya Machimboni Raphael Kalinga aliwaambia Waandishi wa Habari kuwa  Askari Polisi huyo akiwa na kundi la majambazi wenzake ambao idadi yao hakufahamika walifika kijijini hapo kwa lengo la kumvumia na kumpora kwa kutumia mapanga na shoka  mfanya biashara wa Madini ya dhahabu na mashine za kusaga  aitwaye  Daniel  John.
 Alisema  baada ya kuwa wamefika nyumbani kwa mfanyabiashara huyo walivunja mlango  wa mbele wa  nyumba ya  mfanya biashara huyo ambae alikuwa amelala ndani ya chumba chake .
Majambazi hao baada ya kuvunja mlango waliingia ndani  na  mfanya biashara huyo aliwauliza kuwa wao ni akinanani  na ndipo walipomwamuru  kuwa asipige kelele na anyamaze kimya vinginevyo watamuuwa.
Diwani Kalinga ambae ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimmbo  alieleza  ndipo  Daniel  John alipojiandaa na kuchukua bunduki yake ya Shorti gani na kufyatua risasi ambayo ilimpiga Askari Polisi huyo katika sehemu ya kifuani na mgongoni na kufa hapo hapo .
 Alisema majambazi wenzake ambao walikuwa na silaha za jadi baada ya kuona mwenzao kapigwa risasi na kufa waliamua kumbeba marehemu na kwenda kumtupa kichani umbali wa mita 200 kutoka kwenye eneo la tukio na kisha walitokomea kusiko julikana.
Wakazi wa Kijiji hicho walifika nyumbani kwa  mfanyabiashara  huyo na kukuta michirizi ya damu na ndipo walipoamua kuifuata iliko kuwa inaelekea.
Alisema wanakijiji waliendelea kuifuata michirizi ya damu na ndipo walipofika umbali wa mita 200 kutokea nyumbani kwa  Daniel John waliweza kuuwona  mwili  wa Askari Polisi ambae alikuwa tayari amefariki Dunia  na ndipo taarifa zilipotolewa kwa jeshi la polisi Wilaya ya Mpanda.
Polisi walifika kwenye eneo hilo baada ya muda  mfupi na  ndipo walipoweza kumtambua marehemu  kuwa ni Askari polisi wa kituo cha polisi cha Wilaya ya Mpanda .
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha kutokea kwa tukio la askari huyo kuuwawa kwa kupigwa risasi wakati akiwa anataka kufanya ujambazi na kupora .
Alisema mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda .
Kabla ya tukio hilo kulikuwa na  malalamiko  kutoka kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi waliokuwa wakiwatuhumu baadhi ya askari wa Jeshi la polisi kuhusika katika matukio mbalimbali yaliyakuwa yakitokea ya ujambazi na uporaji katika maeneo ya Mkoa wa Katavi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa