Home » » WAWILI WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO YA MILIONI 60

WAWILI WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO YA MILIONI 60

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Jeshi  la Polisi  Mkoa wa  Katavi linawashikilia  watu  wawili  wakazi wa  Tarafa ya Mpimbwe   Wilaya ya Mlele  Mkoani  hapa  kwa tuhuma za kukamatwa na  meno ya Tembo  manne yenye  uzito wa Kirogramu 47.6 yenye  thamani ya shilingi milioni 60 wakiwa wameyabeba kwenye Pikipiki
 Watuhumiwa hao waliokamatwa  walitajwa kuwa  ni  Jastine  Bruno (50) na  Philiberti  Leo (Uliza)  35  Wakazi wa  Kata ya Usevya  Tarafa ya Mpimbwe  Wilaya ya Mlele
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi  Dhahiri Kidavashari  aliwaambia Waandishi wa Habari   jana  kuwa   watuhumiwa hao walikamatwa  hapo   juzi  majira ya saa moja na nusu  huko  katika  Kitongoji  cha  Tompola  Kata ya  Usevya
 Alisema   kabla ya kukamatwa kwa Watuhumiwa hao  jeshi  la Polisi  na  Askari wa Hifadhi ya Taifa   mbuga ya  Katavi  walipata  taarifa kutoka kwa Raia  wema  kuwa watuhumiwa hao wamebeba meno ya  Tembo  kwenye Pikipiki
Kamanda  Kidavashari  alieleza kuwa   baada ya kuwa  taarifa  hizo zimefika kwa Askari wa Tanapa  Katavi na Jeshi la Polisi walishirikiana kuandaa mtego wa kuwakamata  watuhumiwa hao wawili
 Alisema ndipo walipoweza kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa wamabeba  meno  hayo ya Tembo  kwenye Pikipiki  yenye  Namba za usajiri  T 645 CUS  aina ya Toyo wakiwa wameyahifadhi kwenye  mfuko wa    Salpheti
Baada ya  kuwakamata   waliweza kuwepekua na ndipo walipo wakuta  watumiwa wakiwa na meno  hayo ya Tembo  manne  wakiwa wameyahifadhi  kwenye mfuko
Kamanda  Kidavashari  alisema watuhumiwa hao  wote wawili wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi   na wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani upelelezi utakapo kuwa umekamilika
Pia  amewataka  Wakazi wa Mkoa wa Katavi kuendelea na ushirikiano kwa jeshi la Polisi kwa kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo viovu

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa