Home » » AFA BAADA YA KUNYWA POMBE NYINGI KUPITA KIASI BILA KULA CHAKULA

AFA BAADA YA KUNYWA POMBE NYINGI KUPITA KIASI BILA KULA CHAKULA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mkazi wa   Mtaa wa Mapinduzi  Kata ya Ilembo Wilaya ya Mpanda  Omari Salehe(35) amefariki Dunia baada ya kunywa pombe  nyingi  kupita kiasi bila kura  chakula
Kwa mujibu wa majirani wa marehemu huyo  ambao hawakutaka  majina yao kutajwa gazetini  walisema kuwa  marehemu huyo alifariki  Dunia hapo  jana  majira ya saa sita  mchana  nyumbani kwake  katika Mtaa wa Mapinduzi
 Walisema kuwa siku moja kabla ya kifo hicho  marehemu  alishinda kutwa nzima kwenye klabu kinachouza  pombe ya kienyeji aina ya komoni
Siku   hiyo  baada ya kunywa  pombe nyingi kupita kiasi   bila kura  alijikuta  ameshindwa  kuingia   ndani ya nyumba yake  ambayo alikuwa akiishi peke yake  na  badala  yake  alilala  nje ya  nyumba yake  hadi  ambapo  aliamushwa na  majirani zake walipita jirani na  nyumba yake siku iliyofuata majira ya saa  moja asubuhi
Baada ya  marehemu kuamshwa na  majirani  zake  aliingia  ndani ya  nyumba yake   na kisha  alitoka na kuelekea katika  ofisi  ya Mtendaji  wa Mtaa kusikiliza  shauri lale  la kuhusiana na  mgogoro wa kiwanja huku akiwa ajakula  chakula chochote
 Walieleza mara baada ya kutoka kwenye  shauri hilo  majira ya saa tatu asubuhi  alielekea moja kwa moja kwenye  klabu ya pombe  na kuendelea  kunywa  huku akiwa ajakula chakula chochote 
Marehemu baada ya kuona  amezidiwa na pombe  alizokuwa  amekunywa   aliamua  kurudi  nyumbani kwake na kuingia ndani na kukaa kwenye kiti na  baada ya muda  mfupi akafariki  Dunia
Marehemu Omari Salehe amezikwa jana kwenye  makabuli ya Mwanasega Kata ya Ilembo Wilayani hapa  na kifo hicho kimeleta huzuni kubwa kwa wananchi wa Mtaa huo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa