Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Kavuu Mkoani
Katavi kupitia CHADEMA Laulent
Mangweshi ameahidi kuwa endapo
atachaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kavuu atahakikisha anatowa nusu ya fedha za mshahara wake zitumike
kwa ajiri ya kuokoa kuokoa uhai mama
na mtoto
Mgombe huyo
alitowa kauli hiyo hapo jana wakati
alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari
katika Kijiji cha Majimoto Wilayani
Mlele
Mgombea ubunge
huyo alisema wanawake wangi na
watoto wachanga wanapoteza maisha kutokana
na ukosefu wa huma za afya kuwa
mbali na wanako ishi
Alisema
kutokana na hari hiyo ndio maana
kwenye mikutano yake ya kampeni za
kugombea ubunge wa jimbo la Kavuu swala la uhai wa mama na mtoto amelipa
kipaumbele cha kwanza na hata kwenye mabango yake ya kampeni ndio
maana ameandika atahakikisha ana ukoa vifo vya mama na mtoto mchanga
Alifafanua
kuwa endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa
Jimbo hilo atatowa nusu ya fedha za mshahara wake zitumike kwa
ajiri ya shughuli za kuokoa uhai wa mama na mtoto mchanga na pia
atahakikisha ananunua gari kwa ajiri ya
wajawazito na watoto wachanga
Alisema kwenye jimbo lake ataakikisha akina baba na akina mama
wana wanapatiwa elimu ya uzazi wa mpango kabla hawaja anza kutumia dawa
za uzazi wa mpango kwani wapo baadhi ya
akina mama wamekuwa wakipewa dawa za uzazi wa mpango na wamekuwa hawazitumii
kwa ajili ya kukosa elimu
Mangweshi alieleza kuwa atajitahidi kuondoa tatizo la
wasichana kupata mimba wakiwa na umri
mdogo kwa kuishauri Wizara ya Elimu
kujenga mambweni kwenye shule
zote za kata kwa wanafunzi wakike
itakuwa kwake ni mwiko kuishi kwenye nyumba za kupanga jijijini ambako wanaishi bila uangalizi wa wazazi na
waalimu
Nae mgombea wa ubunge wa jimbo la Kavuu
kupitia chama cha ACT Wazalendo Tanzania Sintansilau Kisesa yeye ameleza kuwa endapo atachaguliwa
kuwa mbunge wa jimbo hilo ataakikisha vituo vya afya na zahanati
zinaimalishwa ili akina mama na watoto
wewe wanapatiwa huduma bora zitakazo
wawezesha kuokoa uhai wao
Pia ataishauri
Serikali na Halmashauri yake itenge
bajeti ya Afya ya kutosha ili
kusiwepo na tatizo la upungufu wa
dawa na
vifaa kwenye vituo vya afya na
zahanati kwenye jimbo lake
Alisema
ataweka utaratibu wa kutolewa kwa kwa elimu ya uzazi wa mpango kwenye jimbo lake kwa njia ya
sinema na vipeperushi
Na
atahakikisha kwenye vituo vya afya
huduma ya upasuaji inatplewa kuliko
ilivyo sasa ambapo huduma hiyo ya upasuaji inatolewa katika Hospitali ya Wilaya
ya Mpanda hali ambayo imekuwa ikisababisha wanawake kupoteza maisha kwa kuchelewa
kufika Hostalini kutona na umbali
Pia ataishauri Serikali ipige marufu wasichana
wote wenye umri wa chini ya miaka 19 kuingia kwenye nyumba za kulala wageni
kwani zimekuwa zikichangia wasichana kupata mimba zembe
0 comments:
Post a Comment