Home » » MGOMBEA UBUNGE UKAWA APATA KICHAPO NA GARI YAKE YASHAMBULIWA KWA MAWE

MGOMBEA UBUNGE UKAWA APATA KICHAPO NA GARI YAKE YASHAMBULIWA KWA MAWE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na   Walter Mguluchuma
Katavi
Mgombea Ubunge wa vyama vinavyounda umoja wa   Ukawa(CHADEMA)   wa  Jimbo la  Mpanda  vijijini  Mussa   Masanja  Kantambi  amepata  kipigo na gari yake kushambuliwa kwa mawe na kujunjwa kioo cha mbele baada ya kupita kwenye eneo walilokuwa wakifanyia mkutano wa kampeni za Mgombea Ubunge wa CCM
Tukio la  kupingwa kwa mgombea  huyo lilitokea  hapo  juzi  majira ya saa sita mchana   katika  eneo la  Santamaria Katika  Mtaa wa Mwamkulu  Manispaa ya  Mpanda  Mkoa wa Katavi
Siku  hiyo ya  tukio   Massanja  alikuwa  akitokea   mjini  Mpanda  akiwa  na  gari  lake  aina ya Land Cruiser yenye   namba za usajiri  T390 ANM  huku  akiwa  anaelekea  kwenye  kijiji  cha  Kabage   kwa lengo la kwenda kufanya  mkutano wa kampeni ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Mpanda  vijijini
Wakati akiwa amefika  kwenye  eneo  hilo  la  Santamaria  alikuta  mgombea  Ubunge wa  Jimbo la  Mpanda  Mjini   Sebastiani  Kapufi(CCM) akiwa  anafanya  mkutano wake wa kampeni  za ubunge wa jimbo la Mpanda Mjini
Mgombea huyo wa Ukawa   baada ya kuwa amefika kwenye  eneo hilo la mkutano wa mgombea wa CCM alisimamisha  gari  lake  karibu  na eneo hilo la mkutano kwa kile alichodai kuwa  ameshindwa kuendelea na  safari yake  kwa vile  barabara ambayo alitaka kupita imefungwa na watu waliokuwa kwenye mkutano huu
Kitendo  hicho cha kusimamisha  gari  karibu na mkutano huo kiliwakasilisha wafuasi wa CCM na kuamua  kutoka kwenye  mkutano na kwenda kumvamia   mgombea huyo wa Ukawa na kuanza kumpa kipigo
 Baada ya  kuona kichapo kimezidi  mgombea huyo  alitimua mbio na kwenda kujihifadhi  kwenye  nyumba  moja iliyokuwa jirani huku baadhi ya wafuasi wa CCM wakiwa wanalishambulia gari lake kwa mawe na kulivunja kioo cha mbele
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi  Dhahiri  Kidavashari  amekiri kutokea kwa tukio hilo  hapo juzi  katika  eneo la  Santamaria  Mtaa wa Mwamkulu
 Alisema tukio hilo lilitokea  ila  viongozi wa vyama  hivyo waliamua  kumaliza  tatizo hilo wao wenyewe kwa kufanya mazungumzo  baina yao
Pia   alisema jeshi la Polisi  Mkoa wa Katavi limeandaa mkutano hapo septemba 25 unakao wahusisha viongozi wa  madhehebu yote ya dini , viongozi wa vyama vya siasa na wazee  mashuhuri  ili kujadiliana  na mmna  ya kudumisha  amani katika  kipindi hiki  cha uchaguzi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa