Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi yetu Blog
Wananchi
waliokuwa Raia wa Nchi ya Burundi ambao wamepewa Uraia na Serikali ya
Tanzania hivi karibuni
wanaishi katika Makazi ya Katumba na Mishamo Mkoani Katavi wamehaidi kupigia
kura mgombea wa Urais(CCM)
Dk John
Magufuli wakati wa uchaguzi mkuu wa oktoba 25
Raia hao wapi
walitowa ahadi hiyo kwa
wakati fofauti hapo jana kwenye
mikutano ya hadhara ilifanyika kwenye kijiji cha Kanoge makazi ya wakimbizi ya Katumba na Mishamo
wakati walipokuwa wakitutubiwa na
mgombea Urais(CCM)
Wananchi
walimweleza mgombea huyo
kuwa wanatambua na kuthamini
jitihada zilizofanywa na CCM
hadi wakakubaliwa kupewa uraia
Watanzania
Katika hotuba yake Magufuli aliwaeleza
Wananchi hao kuwa Serikali ya
Tanzania imewapatia Uraia hivyo
watambue kuwa maisha yao yote kwa sasa
yatakuwa Tanzania
Hivyo wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ilikujiletea
maendeleo yao na Nchi kwa ujumla na
endapo atachaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano serikali yake
itawatatulia kero walizo nazo
Kwa upande Mjumbe wa Kamati ya CCM ambae pia Waziri Mkuu
Mizengo Pinda alieleza kwenye mikutano hiyo ya
hadhara kuwa Serikali ya CCM
ilikubali kuwapatia Urai wa Tanzania
waliokuwa Raia wa Burundi ambao kwa hiyari yao wenyewe waliomba kuwa
Raia wa Tanzania
Katika zoezi lililofanyika hivi
karibuni walikuwa Raia wa Burundi
112,000 walikuwa wakiishi kwenye makazi
ya wakimbizi ya Katumba na Mishamo
Mkoani Katavi walipewa vyeti vya
uraia wa Tanzania
0 comments:
Post a Comment