Home » » WANANCHI WAVAMIA KITUO CHA POLISI WATAKA KUKICHOMA MOTO BAADA YA MWENYEKITI WAO KUKATAA KUWATAMBUA WACHAWI‏

WANANCHI WAVAMIA KITUO CHA POLISI WATAKA KUKICHOMA MOTO BAADA YA MWENYEKITI WAO KUKATAA KUWATAMBUA WACHAWI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Watu   sita wakazi wa Kijiji  cha  Ikola  Wilaya ya  Mpanda  Mkoa wa  Katavi  wanashikiliwa  na  jeshi la  Polisi  kwa tuhuma za kuvamia  kituo cha  Polisi cha  Ikola  na kutaka kukichoma  moto  huku wakiwa na silaha za  jadi   baada ya kukasilishwa  na  kitendo cha  Mwenyekiti wao wa kitongoji  cha  Mpalamawe B kukataa kuwatambua  watu  waliotajwa  majina yao kwenye mkutano wa hadhara kuwa ni wachawi (washirikina)
Kamanda wa  Polisi wa Mkoa wa Katavi  aliwaambia waandishi wa  habari  jana  kuwa  tukio  hilo  lilitokea  hapo  juzi   majira ya saa kumi jioni  Kijijini  hapo
 Aliwaja watuhumiwa wanao  shikiliwa na  jeshi la  Polisi  kuwa ni  Pascal  Dominiki( 30, Mirambo  Kasimu  wa  Kijiji   cha Ikola  Wilaya ya  Mpanda
Nikwamba siku  moja ya tukio  hilo  kilifanyika  kikao  cha  Baraza  la wazee wa Kitongoji  cha  Mpalamawe  B  kilichohusishwa  na  imani za  ushirikina   wa kujadili vifo vya watu ambavyo vimekuwa vikitokea  hivi  karibuni  na  katika  kikao  hicho  mwenyekiti wao wakitongoji  Hilali  Rashid   alikuwa ni mjumbe wa kikao hicho
Kamanda  Kidavashari  alisema  Baraza  hilo  baada ya kujadiliana kwa muda mrefu  walibuliana kwamba kwakuwa jambo hilo  la imani za ushirikina  linagusa watu wengi kwenye kitongoji hicho Wazee hao walimuagiza mwenyekiti  kuitisha mkutano wa wananchi wote   ili  kuweza kuwabaini wahusika
 Ndipo  hapo juzi  kilifanyika kikao   hicho cha wananchi wote  na  kwenye kikao  hicho walikuwa wamemualika na  mwenyekiti wa  Kitongoji cha jirani cha Mpalamawe A  Lucas  Mbutulo
Kidavashari  alisema mara  baada ya kikao  hicho  kuanza  Mwenyekiti wa Kitongoji  cha  Mpalamawe  A LucasMbutilo  alidakia  na kumtaja  wananchi mmoja  aliyekuwepo  hapo   Lutha  Wilisoni kuwa ndio  mchawi  ambae amekuwa akisababisha vifo vya watu kwenye  kitongoji hicho
Mwenyekiti wa  Kitongoji  cha  Mpalamawe  B  Hilali  Rashid  alimkaza    Mwenyekiti wa Kitongoji cha  Mpalamawe A   kutaja   majina ya watu   hadhalani  kuwa  ni wachawi kwani anaweza kusababisha  hari ya uvunjwaji wa amani
Kamanda  Kidavashari   alisema  kitendo hicho  cha kumkataza  Mwenyekiti wa Kitongoji  cha Mpalamawe A asiendelee kutaja  majina ya watu anao wadhania kuwa ni wachawi  kitendo hicho kiliwakasirisha wananchi hao  na kuanza kumshambulia  Mwenyekiti wao wa Kitongoji cha  Mpalamawe B kwa kutumia  silaha za jadi
 Askari  Mgambo zaidi ya 20 wa Kijiji  cha  Ikola  walifika kwenye  eneo hilo la mkutano  na kumwokoa  Mwenyekiti huyo  na kumkimbiza  hadi kwenye  Kituo cha Polisi  cha Ikola  kwa lengo la kumuhufadhi kwenye usalama  zaidi
 Alisema kundi kubwa la watu ambao walikuwa kwenye mkutano huo  liliamua kwenda  na walifika kwenye kituo cha Polisi  cha Ikola  kwa lengo  la kutaka kuvamia na kuchoma moto kituo hicho cha polisi   ili  waweze kumpata  Mwenyekiti huyo na kisha wamuuwe
Zoezi hilo  hata  hivyo  halikuweza kufanikiwa kwani lilizimwa na  Askari  Polisi wa kituo  hicho  kwa kushirikiana  na   Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  Delti ya  Ikola
Alisema katika tukio hilo   Lutha  Wilison i  ambae  alitajwa kuwa ni  mchawi  alijeruhiwa  kwa kupigwa  na  rungu   na fimbo  kichwani  na  alikimbizwa katika   Kituo  cha  afya cha Ikola  ambako  amelazwa   na  anaendelea kupatiwa matibabu huku hari yake ikiwa ni mbaya
Kamanda Kidavashari alisema watuhumiwa sita ambao wanashiliwa na jeshi la polisi wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani wakati wowote   mara baada ya uchunguzi kukamilika

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa