Home » » RUSHWA SECTA YA ELIMU NI TATIZO SUGU

RUSHWA SECTA YA ELIMU NI TATIZO SUGU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na  Walter  Mguluchuma 
Katavi
Kutokana  na  Rushwa  kuonekana   kuwa  ni  kikwazo  katika     maboresho ya  sekta ya   Elimu   na  sekta  nyingine  hapa   Nchini   kwa ujumla  Serikali  imekuwa  akifanya  jitihada  za kuhakikisha  hali ya  Rushwa  inakabiliwa  hapa   Nchini  Tanzania
Hayo  yalisema  hapo jana  na  Afisa  kutoka  ofisi ya  takukuru  Mkoa  wa  Katavi  John  Punju  wakati  akiwa  mada  Rushwa  katika  sekta  ya  Elimu  na  athari  kwenye  mkutano wa  waalimu wa  shule  zote za  Msingi  za  Manispaa ya  Mpanda  uliofanyika  katika  shule ya Sekondari ya Mtakatifu  Maria  mjini hapa
Alisema  Serikali  imekuwa ikifanya  jitihada kubwa za kuhakikisha  hari ya  Rushwa  inakabiliwa na kutokomezwa  hapa  nchini
Ambapo  sheria  mwaka 1971  Sheria  ya  kuzuia  Rushwa   NA 16 ilitungwa ikifuatiwa  na  kikosi  cha kuzuia Rushwa  kilianzishwa mwaka 1975 kutokana na utumishi wa umma kupanuka  na watumishi kwenda  kinyume  na  maadili   ya kazi  kwa kutumia  nafasi zao  kama kitega uchumi  kutokana na hari ngumu  ya uchumi  inayoikabili Taifa  katika kipindi hicho
John  alieleza    kuwa  mbali  na  kutunga   sheria   hiyo   na  kuundwa  kwa kikosi  cha kuzuia Rushwa  Serikali  inaendelea  kufanya jitihada   mbalimbali  ikiwa  ni pamoja  na kutunga  sera  na  sheria
Alifafanua  kuwa ilikupambana na Rushwa  serikali  ilianzishwa  mwaka 1996 tume  ya  Jaji  Warioba  ambayo imeonekana kuwa na mwanga  wa mapambano dhidi ya Rushwa  kwa kipindi hiki  kutokana  na taarifa  hiyo  ya tume  baadhi ya viongozi  wa ngazi za juu  Serikalini  waliondolewa kwenye  nafasi zao  na pia taasisi  ya mapambano  dhidi ya   rushwa  imeimalishwa
Alisema athari za  rushwa ziko  nyingi   sana  ambapo  alizitaja  baadhi ya   athari  hizo kuwa ni  Rushwa inachangia  watu kuongozwa na watu wasio na sifa  na  pia inapunguza  uwajibikaji  katika  kazi
Afisa  huyo wa TAKUKURU alitaja  athari nyingine kuwa ni  Rushwa inachangia kushuka kwa Elimu na pia inasababishia watu vifo na kuipotezea  Serikali  pesa  nyingi
Nae  Afisa  Elimu wa Manispaa ya Mpanda  Vicent  Kayombo alisema kuwa  waalimu ni wadau wakubwa  katika  mapambano  dhidi ya  Rushwa  hapa  nchini
Alisema kitendo cha mtu kukataa kutowa taarifa kwa TAKUKURU  anapohitajika kufanya  hivyo ni kosa la jinai
Hivyo  Kayombo  aliwataka waalimu wa Manispaa hiyo kutowa  ushirikiano kwa TAKUKURU pindi wanapo kuwa wanahitaji  taarifa
 Alisema   pia  elimu hiyo iliyotolewa kwa waalimu  na  Afisa wa TAKUKURU itasaidia sana kwenye jamii kwani  mwalimu mmoja  anao   uwezo  wa kuelimisha watu zaidi ya elfu moja  madhara ya Rushwa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa