Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Taasisi ya
kuzuia na kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) Mkoa wa Katavi imemfikisha katika
mahakama ya Wilaya ya Mpanda na kumfungulia mashitaka mzee wa baraza wa Mahakama ya mwanzo ya Mpanda Anna Mlugala kwa
tuhuma za kosa la kuomba na kupokea rushwa ya shilingi laki moja kinyume na
kifungu cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Na11 ya mwaka 2007
Mkuu wa TAKUKURU wa Mkoa wa Katavi john Minyenya aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mhumiwa
alikamatwa hapo mei 21 mwaka huu
katika eneo la Mtaa wa Makanyagio Mjini hapa kufutia mtego ulikuwa umaandaliwa
na TAKUKURU
Alieleza mshitakiwa
kwa kutumia nafasi yake ya uzee wa baraza wa Mahakama ya mwanzo anadaiwa
kutenda kosa la kumshawishi na
kumwomba rushwa ya shilingi laki moja kutoka kwa msiri mmoja
ili aweze kutowa
upendeleo wa kumsaidia katika kesi
yake Na 21\2015
Alieleza
baada ya TAKUKURU kupata taarifa
hizo ilianza kufanya uchunguzi wa awali na ndipo waliweza kubaini tuhuma hizo
ni za kweli
Minyenya alisema
uchunguzi huo uliofanywa uliweza
kuthibitisha kuwepo kwa kesi hiyo
na kwamba mshitakiwa Anna Mlugala
alikuwa na na mawasiliano na msiri
Ndipo terehe
21 mei
TAKUKURU waliandaa mtego wa
Rushwa dhidi ya mshitakiwa
na waliweza kumkamata huko katika
Mtaa wa Makanyagio mjini hapa
Alieleza
baada ya mtuhumiwa
kufikishwa mahakamani alisomewa
mashitaka yanayo na alikana mashitaka dhidi yake ambapo dhamana ilikuwa wazi na mshitakiwa aliweza kutimiza
masharti ya dhamana na
yuko nje hadi hapo kesi yake
itakapo tajwa tena june 6 mwaka
huu
TAKUKURU Mkoa wa
Katavi inatowa wito kwa wananchi kuzingatia
maadili na kutojihusisha na
vitendo vya Rushwa wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku
na wakati wanapo dai haki
zao kwani Rushwa
ni adui haki hivyo haikubaliki
0 comments:
Post a Comment