Home » » WATU WATATU WAKAMATWA NA GOBOLE‏

WATU WATATU WAKAMATWA NA GOBOLE‏


Na  Walter   Mguluchuma 
Katavi
 Watu watatu   Charles  Manyanye (55)  Jacob  Charles (28) na  Mussa Mwigize (30) wakazi wa  Kitongoji  cha  Kamigusu  Wilaya ya Mpanda  wamekamatwa  kwa tuhuma za  kukutwa   wakiwa na  silaha mbili Bunduki aina ya  Gobole wanazimiliki kinyume cha sheria
 Watuhumiwa  hao wote watatu  walikamatwa  machi 28  mwaka huu majira ya saa  kumi na  moja  jioni  huko  katika Kitongoji cha  Kamigusu   Wilaya  ya   Mpanda
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi  Dhahiri  Kidavashari  alisema  watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia msako  unaofanywa na jeshi la polisi Mkoa wa Katavi  dhidi  ya watu wanao miliki silaha kinyume  cha  sheria
 Alisema  kabla ya Polisi kuwakamata watuhumiwa hao  jeshi hilo lilikuwa  limepata taarifa  kutoka kwa Raia  wema  kuwa kuna watu watatu wanamiliki silaha  isivyo  halali kwenye Kitongoji cha Kamigusu
Kidavashari  alisema mbele ya waandishi wa habari  ndipo  hatua za haraka  zilichukuliwa  kwa polisi kufika   Kijijini hapo   kwenye nyumba za watuhumiwa hao watatu
 Alisema    baada ya  kufika  polisi walipofanya  upekuzi kwenye  nyumba  walizokuwa  wakiishi watuhumiwa   na waliweza  kuwakuta watuhumiwa  wakiwa  na silaha  mbili   bunduki aina  ya Gobole  moja ikiwa imefishwa  juu ya dari  na nyingine kwenye  uvungu wa kitanda
 Kamanda Kidavashari alieleza  watu  wote watatu  bado wanaendelea  kushikiliwa na polisi kwa  mahojiano zaidi  na wanatarajiwa kufikishwa  mahakamani mara baada ya uchunguzi utakapokuwa umekamilika

    


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa