Home » » RC AZINDUA MPANGO WA HUDUMA YA UZAZI WA MPANGO

RC AZINDUA MPANGO WA HUDUMA YA UZAZI WA MPANGO




Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Dr  Ibrahimu Msengi amezindua  mradi  wa huduma ya uzazi wa  Mpango  inayotolewa bure na   Marie  Stopes   Tanzania (MST) kwa  Wananchi wa Mkoa wa Katavi
Uzinduzi huo uliohudhuliwa na maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Katavi ulifanyika jana katika uwanja wa shule ya Msingi   Kashaulili  mjini Mpanda ambapo kaimu   Mkuu wa Mkoa ambae  ni  mkuu wa Wilaya ya Mpanda  Paza  Mwamlima alizindua  huduma  ya mpango huo kwa niaba ya   Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Dr Ibrahimu Msengi
 Dr Msengi  katika   hotuba yake   alisema kuwa  uzazi wa  mpango ni hiari  ambao mtu  au wanandoa  wanaamua  idadi  ya watoto  watakao zaa kwa mpangilio  uliokubalika  kwa ajiri ya afya zao
 Alisema huduma hiyo ya mpango wa  uzazi  iliyozinduliwa  katika Mkoa wa Katavi  mpango huo  utasaidia  kupunguza vifo  vya akina Mama  na watoto katika Mkoa wa Katavi  na watoto  chini ya umri  wa miaka mitano  ikiwa ni katika  kutimiza   malengo ya milenia  namba  nne   na namba   tano
Alifafanua  zaidi  ya  wanawake  elfu nane hufa  hapa  nchini kila mwaka kutokana na uzazi   na kinachoshangaza  wanawake  walioolewa  ndio  wengi wao  wamekuwa  wanashindwa  kupata huduma ya uzazi wa mpango
Alisema  wananchi wa  Mkoa wa Katavi  watumie  fursa  hiyo   kuwahamsisha watu  watumie  njia za  uzazi wa  mpango  kwani ni salama
 Dr Msengi aliwataka  wananchi  wawatumie  wataalamu  ili  waweze kuwapatia  ushauri  na  kuwaelimisha  umuhimu wa uzazi wa mpango  na kuwapuuza  watu  ambao  wanatafsiri    vibaya   huduma ya  mpango wa uzazi  na   wanaopinga  uzazi  wa mpango
 Aliisema  kumekuwepo  na  imani potofu  na taarifa  zisizo sahihi  kuhusu  uzazi wa   mpango  ambazo  zimesababisha  kina mama  wengi  kuwa waoga  wa kutumia  njia  hizo  na kishia  kushika mimba  zisizotarajiwa
Kwa  wanaume  njia ya  za uzazi  wa mpango  ni  chache  kwa hiyo  fursa  ya kushiriki  ni ndogo  ukilinganisha na wanawake  hata hivyo  kuna baadhi ya wanaume  huwazuia  wake zao  kutumia uzazi wa mpango kufanya hivyo  ni  kutomtendea haki mwanamke
 Alisema wanaume wamekuwa wakidhani kuwa jukumu la  kunga kizazi na  mpango wa  uzazi ni  kwa ajiri ya mwanamke tuu wakati jukumu hilo ni la mwanaume na mwanamke  hivyo    huduma hiyo waakikishe inawafikia wananchi wote wa Mkoa wa Katavi hata yale maeneo ambayo yamekuwa yakifikika kwa shida kama vile Ilunde Bugwe, Mnyagala ambako unakuta mtu mmoja anakuwa na watoto 40 wa kuzaa mwenyewe na wake zaidi ya watatu
Nae  Mkurugenzi wa Rasilimali watu  wa Marie  Stopes  Tanzania  Eliy  Reweta  alisema pamoja  na kuendeleza  kazi zilizokuwa  huko nyuma   timu   za utoaji huduma zimeongezwa  katika mikoa ya  Singida , Kilimanjaro ,Manyara  na  Katavi  lengo ni kumfanya  kila mtu  achague  njia ya uzazi ya mpango anayohitaji
 Alisema  huduma  zinazo tolewa  kupitia  shirika la Marie  Stopes  Tanzania zinachangia  asilimia ishirini na tano  yahuduma  zote za  mpango  wa uzazi  ukiondoa kondomu
 Alifafanua kuwa huduma  ya uzazi wa mpango hutolewa na  timu ya  wataalamu  wa uzazi wa mpango  waliopitia  mafunzo  maalumu  na kila timu inagari  linalozunguka  na kutowa huduma  hizo  katika Zahanati  na  vituo  vya afya  vilivyoko  katika  maeneo ya vijijini  kwa siku 21  kila mwezi
Nandio maana kwa kutambua umuhimi huo Marie  Stopes  imekabidhi gari jipya wakati wa uzinduzi huo kwa ajiri ya Mkoa wa Katavi litakalo saidia kutowa huduma na kuwafikia  kila mtu mahari pale alipo alisema   Elly
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Enock Gwambasa alieleza  kuwa mpango huo utasaidia  kuwafanya watu  waweze  kuwa na utatatibu mzuri wa  kuzaa watoto kwa mpangilio  kuliko iliyo sasa
 Alisema Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa miwili  inayoongoza kwa kuwa  na ongezeko kubwa la watu  ikiwa inaufuatia Mkoa wa Dares  salaam
 Kwa upande wake  mrembo wa  mashindano ya Miss  Marie Stopes  Tanzania  Doreen  Benne  alisema kuwa  uzazi wa mpango  unamkinga mtu  kupata mimba  zisizotarajiwa  na kumwepusha  na kuingia kwenye mtego wa kutoa mimba  kusiko salama
Pia  wanawake wengi  kwa sasa kupitia mpango huo wa uzazi  wanafanikiwa kumaliza masomo  yao  na kutengeneza maisha  kabla ya  kuanza  mpango wa  kutengeneza familia
       
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa