Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi yetu blog
Mwanamke mmoja
Mkazi wa Kitongoji cha Mtisi Kata ya Sitalike Wilaya ya
Mlele Mkoa wa Katavi amejinyonga
hadi kufa kwa kutumia kitenge
chake kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari
aliwaambia waandishi wa habari kuwa mwanamke huyo aliyejinyonga hadi kufa alifahamika kwa jina la
Milembe Charles (25) Mkazi wa Kitongoji cha Mtisi.
Alisema tukio la mwanamke huyo kujinyonga lilitokea
hapo jana majira ya saa kumi na mbili jioni
katika shamba la wazazi wake lililopo kijini hapo.
Alifafanua kuwa kabla ya tukio hilo marehemu alikuwa akiishi
nyumbani kwa wazazi wake baada ya kuwa
wametengana na mume wake ambae walikuwa na ugomvi nae kufuatia mume wa marehemu kuwa na mke mwingine kwenye
Kijiji cha Kasekese kitendo ambacho
marehemu hakuwa ameridhishwa nacho.
Siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa
alikuwa nyumbani kwa wazazi wake
ndipo ilipofikia mida hiyo ya tukio aliondoka nyumbani kwa wazazi wake pasipo
kuwa amewaagakuwa anakwenda wapi.
Alisema wazazi wa marehemu baada ya kuona muda umekuwa mrefu tokea marehemu alipoondoka nyumbani walipata
mashaka na ndipo walipoamua kwenda
nyumbani kwa mume wake kumtafuta hata hivyo mume wa marehemu aliwajibu kuwa
siku hiyo alikuwa haja fika nyumbani kwake.
Jitihada za
kumtafuta ndipo zilianza na ndipo
waliweza kumkuta marehemu akiwa amejinyonga hadi kufa juu ya mti
wa mwembe kwa kutumia kitenge
chake katika kichaka
kilichopo jirani na nyumba ya
wazazi wake.
Kidavashari alisema uchunguzi wa tukio hilo umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni
wivu wa mapenzi kutokana na mume
wa marehemu kuwa na mahusiano ya
kimapenzi na mwanamke mwingine na mwili
wa marehemu umeishafanyiwa uchunguzi wa kidaktari na wamekabidhi
ndugu wa marehemu kwa ajili ya
mazishi.
0 comments:
Post a Comment