Home » » WANAKIJIJI WAVAMIA KAMBI YA KAMPUNI YA UCHIMBAJI WA MADINI WACHOMA GARI MOTO

WANAKIJIJI WAVAMIA KAMBI YA KAMPUNI YA UCHIMBAJI WA MADINI WACHOMA GARI MOTO


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
 Wananchi wa Kijiji cha  Ibindi Kata ya Machimboni Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamevamia kambi ya Kanpuni ya uchimbaji wa madini  ya Sambulu Mining na kuchoma  moto  gari la Kampuni  hiyo na vitu  mbalimbali  baada ya  watumishi wa Kampuni hiyo  kumkamata  mwanajijiji mwenzao  na na kisha  kumkata na panga kwa kumtuhumu  kuiba mawe yanayosadikiwa kuwa na madini ya Dhahabu yenye kilo mbili ya thamani ya milioni 90
Kwa mijibu wa Diwani wa Kata hiyo Raphael Kalinga tukio hilo lilitokea    hapo juzi  majira ya saa kumi na nusu usiku Kijijini hapo
 Siku hiyo ya tukio watumishi wa Kampuni hiyo wakiwa na msimamizi wa Kampuni hiyo  aitwaye  Seif Hamad walifika kwenye Kijiji hicho huku wakiwa wameshika mapanga na kuwafunguza baadhi ya wanakijiji ambao walikuwa wakiwatuhumu  kuwa wamewaibia mawe ambayo wanadai yalikuwa yana madini ya dhahabu kilo mbili
 Katika msako huo walioufanya watumishi hao  waliwajeruhi  wananchi saba kwa kuwakata kata na mapanga katika sehemu zao za mwili
 Baada ya kuwa wamewajeruhi  watumishi hao   walimchukua wanakijiji  mmoja aitwaye Rongino  Petro  na kwenda nae kwenye kambi ya Kampuni hiyo iliyoko  nje kidogo ya  kijiji hicho
 Alisema  wananchi walivyoona mwenzao  amechukuliwa  waliamua kwenda kwenye kambi ya kampuni hiyo huku wakiwa wameongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji  Cristopher Modesti na Mtendaji wake wa Kijiji Sulvia Kampama kwa lengo la kumkomboa mwenzao
 Hata hivyo baada ya kuwa wamefika kwenye kambi hiyo viongozo hao wa Kijiji pamoja na wananchi hao waliambiwa ni marufuku kusogea kwenye eneo hilo na waondoke mara moja
 Diwani Kalinga alieleza baada ya muda mfupi baadaye polisi watatu walifika Kijijini hapo  huku wakiwa na gari lao na  kuwakamata wananchi saba ambao waliokuwa wamejeruhiwa na watumishi hao kitendo hicho kiliwaudhi wananchi wa Kijiji hicho kwa kile walichodai kuwa wananchi hao  hawakuhusikaa na wizi huo
 Alisema wanakijiji  hao walianza kuwashambulia polisi kwa mawe  wakitaka wananchi wenzao waachiliwe  na  polisi walipoona wamezidiwa    waliamua kuondoka kwenye eneo hilo huku wakiwa   wamewabeba  kwenye  gari lao wana kijiji hao saba ambao waliwapeleka kwenye kituo cha Polisi cha Mpanda Mjini
 Kundi kubwa la wanajikiji  baada ya kuona wenzao wembebwa na Polisi  walielekea kwenye Kambi  ya Kampuni hiyo  huku wakiwa wameshika mikononi silaha za jadi  hari ambayo iliwafanya  watumishi wa kampuni ya Sambulu watimue mbio na kuicha kambi ikiwa haina mtu hata mmoja
Alisema wanakijiji hao mbao welikuwa na hasira waliamua kuchoma gari  aina ya Toyota yenye namba za usajiri  T531 AGT na kuiteketeza kabisa kwa moto kila waliharibu vitu mbalimbali vya Kampuni hiyo  na kisha walikwenda kuvitupa na kisha  walitamka  kuwa mwekezaji huyo asionekane tena kwenye Kijiji hicho
Alieleza kuwa katika tukio hilo watu saba wanashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo  ambao ni  Rongino Petro,Sokoni Mteta, Taji Sanane ,Kulwa Jamres,Gabrieshi  Shaulitanga ,Malilo  Pelesiano  na mtu  mmoja aliyefahamika kwa jina la Mussa
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho  Cristophar  Modesti  alisema kuwa wananchi wa Kijiji hicho mara baada ya kutokea kwa tukio hilo wamekimbia familia  zao kwa kuhofia kukamatwa na polisi
Nae Katibu wa  Mbunge wa Jimbo hilo la Katavi Charles Kanyanda  linaloongozwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda alilazimika jana kwenda kijijini hapo na kufanya mkutano na wananchi  ambapo aliwaeleza kuwa kungekuwa na mahusiano mazuri baina ya  wanakijiji na mwekezaji hayo yasingetokea
 Pia aliwaomba wananchi wa Kijiji hicho wapunguze hasira kwa mwekezaji huyo na  aruhusiwe   aendelee kufika kijijini hapo wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiwa bado unaendelea
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Ngemela Lumbinga amekili kupokea taarifa za tukio hilo la wananchi kuvamia kambi hiyo na kuchomwa kwa gari la kampuni hiyo
Alisema anatarajia kufika kwenye eneo hilo  huku akiwa  na Afisa wa madini ilikuweza  kuongea na wananchi wa kijiji hicho cha Ibindi


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa