Home » » RC AGIZA WANAFUNZI WALIOACHA SHULE WASAKWE

RC AGIZA WANAFUNZI WALIOACHA SHULE WASAKWE


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu Blog
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr   Ibrahimu Msengi amewaagiza  wanafunzi wote wa Sekondari ya Mwese Wilaya ya Mpanda walioacha kuendelea  na  masoma kutokana na sababu mbalimbali  ikiwepo ushirikina na kuolewa   warudi sheleni na waendelee na masomo   yao
Mkuu huyo wa Mkoa Dr Msengi alitowa agizo hilo hapo juzi wakati wa kikao chake na waalimu wa shule ya Sekondari ya Mwese kilichofanyika shuleni hapo
Agizo hilo alilitowa kufuatia taarifa iliyotolewa mbele yake na mkuu wa shule hiyo  mwalimu  Yohana Manyanda  ambae alieleza kuwa shule hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa  la utoro wa wanafunzi na kupelekea mabweni ya shule hiyo kuwa wazi
 Alisema  shule hiyo  inayomabweni yanayoweza kutumiwa na wanafunzi wasichana 100 lakini wanafunzi wanaotumia mabweni hayo mawili ni wanafunzi saba na  bweni moja la wanafunzi wavulana lililiopo shuleni hapo lenye uwezo wa kutumiwa na  na wavulana 50 linatumiwa na wanafunzi 13 tuu
Mkuu huyo wa shule  alieleza kuwa utoro wa wanafunzi wa sekondari hiyo  yenye  jumla ya wanafunzi  187 wavulana 85 na wasichana  102 unatokana  na sababu mbalimbali  zinazochangiwa na wazazi wao kuwa na imani za kishirikiana  ambao  wanaamini kuwa watoto wao wakiwa shuleni wataugua ugonjwa wa kuanguka na wengine wameacha masomo na kuolewa
Kufuatia taarifa kutolewa mbele yake Mkuu wa Mkoa  Dr Msengi alisema Serikali haiko  tayari kuona wanafunzi hao wa shule hiyo wanaacha kuendelea na masomo kwa sababu zisizo na msingi
Alisema nawaagiza wanafunzi wote ambao walioacha masomo kwenye shule hiyo  warejee shuleni na baada ya  mwezi mmoja  masako mkali utafanyika kuwasaka na kuwarejesha kwa nguvu wanafunzi wote ambao watakuwa wameshindwa kurejea shuleni na wazazi wao nao watafikishwa mahakamani
Niabu kusikia  wanafunzi wanashindwa  kusoma  shele huku mabweni ya wanafunzi yakiwa wazi wakati  maeneo mangine ya Nchi  wanalilia shule zao kuwa na mabweni
 Alisema agizo lake hilo si lamzaha  na  litaendelea pia  kwa maeneo yote ya Mkoa wa Katavi   na wazazi wa wanafunzi watakao bainika watoto wao wameacha masoma watachuliwa hatua za kisheria kwani taratibu za sheria za kuwashitaki wazazi wao zipo wazi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa