Home » » HOT NUUUZ: MKUU WA MKOA AIGIZA KAMPUNI YA BYTRADE KUMLIPA FIDIA WAZIRI MKUU MH. PINDA KWA KUMUUZIA MBEGU ZA ZA MAHINDI FEKI

HOT NUUUZ: MKUU WA MKOA AIGIZA KAMPUNI YA BYTRADE KUMLIPA FIDIA WAZIRI MKUU MH. PINDA KWA KUMUUZIA MBEGU ZA ZA MAHINDI FEKI


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu Blog
Mkuu wa  Mkoa wa Katavi Dr  Ibrahimu   Msengi  ameigiza Kampuni ya    Bytrade  yenye makao yake makuu Mkoani Arusha  inayowauzia wakulima  mbegu za mahindi hapa nchini aina ya  PIONEER Phb 3253 ameiagiza kampuni hiyo  kumlipa  fidia Waziri Mkuu  Mizengo Pinda    baada ya  kumuuzia mbegu  zisizo kuwa na ubora  zilizoshindwa kuota baada ya kupandwa kwenye shamba lake lililoko Kijijini  kwake  Kata ya Kibaoni Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi
Dr  Msengi alitowa agizo hilo hapo jana   kwenye shamba la Waziri Mkuu Pinda baada ya kulikagua shamba hilo lenye ekari sitini  alipokuwa amefuatana na wataalamu mbalimbali wa kilimo wa  wa  Mkoa wa Katavi kufutia  malalamiko mbali mbali yalikuwa yamepelekwa kwake na wakulima  waliokuwa wamepanda mbegu za kampuni hiyo na kuwa zimeshindwa kuota likiwemo shamba hilo la Pinda
 Awali  Afisa kilimo wa Mkoa wa Katavi Shanal  Nyoni  alimweleza Mkuu huyo wa Mkoa kuwa shamba hilo la Pinda lina ukumbwa wa ekari sitini  ambazo  zimelimwa na kupandwa mahindi kati ya hizo ekari  29 zilipandwa mbegu za mahindi za kampuni ya  Bytrade aina ya  Pioneer  Phb  3253
Nyoni alieleza kati ya ekari hizo ekari tisa zimeshindwa kuota kabisa  kutokana na mbegu hizo kutokuwa na ubora licha ya eneo hilo kupandwa  kwa  usimamizi wa karibu wa wataalamu wa kilimo  ambao hulitumia shamba hilo kama  shamba darasa kwa wananchi wa Kata ya Kibaoni
Alieleza  shamba hilo pia limepandwa  mbegu za mahindi za kampuni ya  Monsanto  aina ya  Dk c 9089 ambao zimeota zenye  bila  shida yoyote ile  tofauti na mbegu hizo
 Alisema tatizo la mbugu za kampuni  hiyo  kupandwa na  kushindwa kuota limetokea pia kwa wakulima wengine wakata za Kibaoni Usevya ,Mamba na Itenka katika Wilaya ya Mlele Mkoani  hapa
 Akitowa agizo  hilo Dr  Msengi alisema  mbegu zilizotumika kupandwa kwenye shamba hazikuwa nzuri  na wala hazikiwa na ubora unasitahili
 Alisema lengo la Serikali ni kumsaidia mkulima ili aweze kuongeza uzalishaji na sio kumfanya mkulima avunjike moyo kwenye jitihada zake za kilimo
  Alifafanua  kuwa Serikali  haitakubali  kuona nguvu za wakulima zikiwa zinapotea bure kwa faida ya watu wachache wanaotaka  kujinifaisha  kwa kuwauzia mbegu mbevu wakulima  na  Serikali ya Mkoa wa Katavi itahakikisha inayathibiti makampuni yote ambayo yanataka kupoteza bure nguvu za wakulima
 Alisema Mkoa wa Katavi  hautasita kuyafutia leseni makampuni yatakayo bainika yanasambaza kwa wakulima pembejeo za kilimo ambazo hazina ubora
Dr  Msengi  aliziagiza Halmashauri zote nne za Mkoa wa Katavi kufanya tathimini ya  mashamba yote ambayo yalipandwa mbegu za kampuni hiyo na zimeshindwa kuota  na wakulima hao walipwe fidia na  kampuni hiyo
Alisema gharama wanayositahili kulipwa ni wakulima wote  na sio Pinda Peke yake na wataalamu hao wazingatie pia na muda waliotumia wakulima pamoja na nguvu zao
 Alisema kwa hilo yeye kama Mkuu wa Mkoa hana wasilaha hata kidogo na uamuzi wake huo hivyo wataalamu wa Kilimo wahakikishe baada ya siku saba wawe wamempa utekelezaji wa maagizo hayo
Kwa upande wake meneja wa mbugu wa kampuni hiyo ya  Bytrade   Rajab  Athuma alimweleza  Mkuu huyo wa Mkoa kuwa tayari kampuni hiyo imeanza kupanda upya mbegu nyingine kwenye shamba hilo la Pinda na tayari wamepanda ekari nne na bado wanaendelea
 Alisema hata hivyo anawasiwasi na utaalamu uliotumika wakati wa kupanda shamba hilo kuwa inawezekana kulikuwa na kasoro
Kauli hiyo ilipingwa vikali na Mkuu wa Mkoa pamoja na afisa kilimo kwa kile walichomweleza  kuwa wakati wa upandaji wa mbegu hizo nawao walishiriki kupanda

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015: JE UNAPENDA NANI AWE KIONGOZI WAKO KATIKA MIAKA 5 IJAYO? JAZA FOMU FUPI HAPA

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa