Home » » INAHUZUNISHA SANA: MSICHANA (16) ACHINJWA, ANYOFOLEWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI, ZIWA NA MIKONO YAKE MIWILI

INAHUZUNISHA SANA: MSICHANA (16) ACHINJWA, ANYOFOLEWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI, ZIWA NA MIKONO YAKE MIWILI


Na  Walter Mguluchuma
Katavi yetu Blog
Mwanamke mmoj aliyetambulika kwa  jina la  Elizabeth Richard(16) Mkazi  wa Kijiji cha Ilalangulu  Kata ya Kibaoni Wilaya ya Mlele  Mkoani hapa  ameuwawa  kikatili  kwa  kuchinjwa  shingo  na kukatwa   ziwa lake la kushoto na mikono  yake  na kisha   kunyofolewa  sehemu zake za siri
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  alisema mauwaji hayo  ya kikatili  ya mwanamke huyo  yalitokea hapo juzi  saa  saa nane mchana kijijini hapo
 Alisema siku ya tukio  marehemu  akiwa na  mumewe aitwaye  Hevinie  Kagembe  waliondoka  nyumbani kwao  majira ya asubuhi  kwenda shambani kwa lengo la kulima shamba  huko katika maeneo ya Kazaroho ambapo wanandoa hao walikuwa wakilima  maeneo tofauti ya mashamba yao
 Hata  hivyo  ilipofikia  majira ya saa kumi jioni  mume wa marehmu Hevinie  alirudi nyumbani kwake  lakini hakuweza  kumkuta  mkewe  kama ilivyokuwa  kawaida  yao ambapo mkewe alikuwa na kawaida ya kutangulia kurudi nyumbani kwa ajiri ya kuandaa chakula
Kamanda Kidavashari alisema  alipofikia majira ya saa mbili usiku mume wa marehemu aliingiwa na shaka kuona hadi majira hayo marehemu alikuwa hajarudi nyumbani wakati sio kwaida yake
Mume  huyo wa marehemu aliamua  kumpigia simu  Mama  mzazi wa marehemu ambae alikuwa akiishi kijijini hapo  ili kutaka kujua kama marehemu mkewe yuko  kwa mama mkwewakehata hivyo  mama  mkwe  alimjibu kuwa  marehemu hajafika nyumbani kwake
Baada ya  majibu hayo kutoka kwa mama wa marehemu  juhudi za  kumtafuta  marehemu  ziliendelea  kwa  taarifa kutolewa  kwa uongozi wa Serikali ya Kijiji hicho  ambao walianza jitihada za kumtafuta kwa kushirikiana na wananchi
 Siku iliyofuata   yaani jana majira ya  saa mbili  asubuhi  mtu mmoja  ambae alipita kwenye shamba alilikuwa analima marehemu  alipoweza  kuuwona mwili wa marehemu ukiwa kando kando ya shamba lake  na marehemu
 Kamanda Kidavashari alieleza  raia mwema huyo  baada ya kuuwona  mwili  wa marehemu  alikwenda kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi kituo cha Kibaoni  kuwa  kuna mwili wa marehemu  umeuona  ukiwa kandokando ya shamba ukiwa umefunikwa
 Baada ya taarifa kufika kwenye jeshi la polisi walikwenda kwenye eneo hilo huku wakiwa na viongozi wa kijiji hicho cha Ilalangulu  na ndugu wa marehemu
Walipofika kwenye eneo hilo  marehemu  alikutwa akiwa amechinjwa chingo  na kichwani akiwa amekatwa na mapanga  na ubongo wake ukiwa umetoka nje  pia  akiwa amenyofolewa sehemu zake za siri  ziwa lake moja la kushoto na  mikono yake yote miwili
 Kamanda Kidavashari  alisema Polisi waliweza kufanya uchunguzi kwenye eneo hilo  ndipo walipoweza  kubaini  kuwa jirani na eneo walilomkuta marehemu  kunadalili za  kuchimbwa   na kufukiwa kitu kwenye eneo hilo
Ndio walipoamua  kufukua eneo hilo  na baada ya kufukua eneo hilo  ndipo walikuta viungo vya mwili wa marehemu   mikono  yake miwili y  ziwa lake moja  na nguo za marehemu zikiwa ndani ya shimo   huku sehemu zake za siri hazikuweza kupatikana kabisa katika eneo hilo
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema  jeshi la polisi  kwa kushirikiana  na uongozi wa  Kijiji hicho  wanaendelea  na msako   mkali  katika maeneo  mbalimbali  ili  kubaini  na kuwakamata   wale wote walihusika  katika mauwaji haya
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa