Home » » AUAWA NA MWILI WAKE KUKUTWA KATIKA KISIMA CHA MAJI

AUAWA NA MWILI WAKE KUKUTWA KATIKA KISIMA CHA MAJI


N a Walter Mguluchuma
Katavi
 Mtu mmoja  aliyejulikana kwa jina la  Mary  Magese (39) Mkazi wa Kijiji cha Itenka  Tarafa ya Nsimbo  Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi  amekutwa akiwa ameuwawa  na  mwili wake kutupiwa kwenye kisima cha maji
Tukio hilo limetokea hapo Septemba 14 mwaka huu majira ya saa mbili usiku kijijini hapo mara baada ya marehemu  kumaliza kula chakula cha usiku akiwa na mume wake  Razaro  Maziku(40)
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema mara wanandoa hao wawili walipomaliza kula chakula  mume wa marehemu   Razaro Maziku alimuga  mkewe kuwa   anakwenda nje  bafuni kuoga  
Alisema  Razaro alipomaliza kuoga  alirudi chumbani kwake ambako alikuwa amemuacha mkewe  na hakuweza kumkuta  mkewe hari ambayo ilimfanya amtafute kwenye maeneo ya nyumba yao waliokuwa wakiishi pamoja
Kamanda Kidavashari alifafanua baada ya kumtafuta kwa muda mrefu bila  kumuona   ndipo mume huyo wa marehemu alipoamua kwenda kumtafuta kwa majirani na kwa ndugu  zake  lakini  hakuwaza kumpata
 Siku iliyofuata  majira ya saa mbili asubuhi  kulizagaa taarifa kuwa  kuna maiti  imeonekana kwenye kisima cha maji huku ikiwa inaelee kwenye maji ya kisima
 Alisemabaada ya taarifa hizo kufika kwenye uongozi wa Kijiji viongozi wa kijiji waliondoka wakiwa wamefuatana na wananchi hadi kwenye eneo hilo la tukio  na kuukuta mwili wa marehemu ukiwa unaelea juu ya maji  na marehemu aliweza kutambulika kuwa  mke wa Razaro Maziku
Kidavashari alieleza   uchunguzi wa awali  umebaini  kuwa chanzo  cha mauwaji  hayo  kimetokana  na wivu wa kimapenzi  baina ya  mume wa marehemu  Razaro Maziku  na Shija  Joseph  ambae alikuwa akituhumiwa kuwa hawala yake na marehemu  wa  muda mrefu  hari ambayo ilikuwa ikiwafanya marehemu kuwa na ugomvi wa mara kwa mara na mumewe
 Alisema jeshi la polisi  linamshikilia  mume wa marehemu kuhusiana na kifo hicho  kwa mahijiano zaidi  na atafikishwa mahakamani  baada ya kuwa  upelelezi  umekamilika
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa