Na Walter Mguluchuma Mpanda Katavi yetu blog
POLISI
mkoani Katavi inawashikilia watu wanne wakituhumiwa kumua kikatili mkazi
wa kijiji cha Kaseganyama, Kata ya Sibwesa
wilayani Mpanda, Salu Kadigosa (65) kwa kumchinja kwa imani za
kishirikina .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo ambapo amewataja watihumiwa
hao kuwa ni pamoja na Masanja Kisatya (32) , Silya Masunga (30) wote
wakazi wa kijiji cha Kaseganyama.
Wengine kwa mujibu w Kamandawa polisi wa Mkoa wa Katavi ni pamoja na Kibya Malongo (27) na Lutelema Mwanza (33) wote wakiwa wakazi wa kijij cha Sibwesa wilayani humo .
Anasimulia
mkasa huo uliotokea Agosti 18, mwaka huu, saa mbili usiku kijijini Kaseganyama,
KamandaKidavashari alida kuwa uchunguzi wa awali umebainisha kuwa marehemu alikuwa
akilalamikiwa na na ndugu zake kwamba ni
mchawi.
Kwa
mujibu wa Kidavashari , mwaka 1993 mtoto wa
marehemu aitwae Masanja Kisatya (32)
alifiwa na watoto wawili , Rebeka Msanja
na Sayi Masanja pia kaka yake mkubwa
alifiwa na watoto watatu , ndipo
wanafamilia waliketi na kuamua kwenda
kwa mganga wa kienyeji .
“Ndipo
mganga huyo wa kienyeji alipomtaja
marehemu kuhusika na vifo vya watoto hao kwa imani za kishirikina”
anadai Malengo
.
Inadaiwa kuwa Agosti 16,
mwaka huu saa kumi na mbili jioni mtu aliyetambulika kwa jina moja la Lugalila , mkazi wa kiji
cha Sibwesa akiwa na mwenzake
wawili ambao hawakufahamika majina yao waliwasili nyumbani kwa Masanja
Kisatya .
Kwa mujibu waKidavashari
muda mfupi baadae wageni hao waliondoka wakiongozana namwenyeji wao Masanja
akiwasindikiza kwenda kuwaonesha
nyumbani kwa Salu Kadigosa kisha Masanja
akarejea kwake .
“Muda mfupi
baadae mauaji hayo ya
kutisha yalitokea na Masanja
lipewa taarifa lakini
hakuchukua hatua yeyote hali iliyoashiria kuwa yeye ndiye aliyehusika kwenye
mauaji hayo’ anadai Malengo .
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment