Home » » AUWA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI WAKATI AKIELEKEA KUNUNUA MAGUNIA YA MPUNGA

AUWA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI WAKATI AKIELEKEA KUNUNUA MAGUNIA YA MPUNGA


Na  Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la  Enock  Lugonda  (35) Mkazi wa Kijiji  cha Mbugani Kata ya Kakese  Wilaya  Mkoa wa Katavi ameuwawa kwa kupingwa na kitu kizito kichwani  na watu wasiofahamika wakati akiwa njiani anaelekea kununua gunia 40 za mpunga
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina mwandamizi msaidizi  Dhahiri Kidavashari  tukio hilolimetokea hapo Agosti 17  majira ya saa saba mchana
Kidavashari alisema siku hiyo ya tukio marehemu  aliondoka nyumbani kwake majira ya saa saba mchana  akiwa na mtu mmoja asiyefahamika  na kuelekea katika  kitongoji cha   Mwagoe  kwa lengo la kwenda kununua mpunga gunia 40
Baada ya kuondoka marehemu hakurejea tena nyumbani  hadi majira ya saa kumi jioni  alipookotwa  akiwa  ameisha fariki Dunia katika eneo  la barabara itokayo  Kijiji cha Kakese kuelekea  Kijiji cha jirani cha Mwamkulu
Alieleza  baada ya marehemu kuokotwa akiwa amefariki Dunia  wananchi walitowa taarifa kwa jeshi la polisi ambao walifika kwenye eneo hilo  na kisha marehemu alifanyiwa uchunguzi wa kidakitari na kubaini kifo chake kilisababishwa na kupingwa na kitu kizito kichwani
Kamanda Kidavashari alisema jeshi la polisi linamshikilia  Mussa Robart (29) Mkazi wa kijiji  cha Mbugani Kata ya Kakese kwa tuhuma za mauwaji hayo
Alieleza kwani ndiye mtu  ambae alikuwa na mahusiano ya kibiashara na marehemu  na ndiye waliyewasiliana na marehemu kwa njia ya simu kuhusiana na biashara hiyo ya mpunga

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa