Home » » Shirika la Walter Red latoa msaada wa pikipikim 24 za thamani ya zaidi ya tsh 52, kwa ajiliya kutolea huduma za Afya

Shirika la Walter Red latoa msaada wa pikipikim 24 za thamani ya zaidi ya tsh 52, kwa ajiliya kutolea huduma za Afya


Na Walte  Mguluchuma 
Mpanda  Katavi
Shirika  la  Walter Red    limetowa msaada  wa Pikipiki 24 zenye thamani ya  Tsh 52,800,000 kwa Halmashauri  za Mkoa wa Katavi kwa ajiri ya kutolea huduma za afya ili kusaidia ufutiliaji  wa wagonjwa  watoro  wanaotumia dawa za  kufubaza  makali ya  Virusi  vya VVU  Mkoani  Katavi
Pikipiki  hizo zilikabidhiwa  mwishoni mwa wiki iliyopita  kwa Halmashauri zote  nne  za Mkoa wa Katavi katika  hafla iliyofanyika   katika  viwanja vya ofisi  za Mkuu wa Mkoa wa Katavi  ambapo mgeni Rasmi alikuwa  ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr  Rajabu Rutengwe
Katika  Risala iliyosomwa na  Mganga  Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr  Yahaya Hussein  kabla ya makabidhiano hayo alisema vitendea  kazi hivyo  vitasaidia  kufanyanyia  kazi katika maeneo  mawili kwa ajiri ya kutolea huduma za Afya
Alisema pikipiki hizo zitawasaidia  ufuatiliji  wa wateja  wanao tumia dawa za  kufubaza  VVU  ambao  watakuwa na kupindi cha miezi mitatu mfululizo  bila kufika kwenye vituo vyao walivyokuwa wakichukulia dawa
Alifafanua lengo ni  kupunguza  na hatimaye  kutokomeza  kabisa  utoro wa  watu wanao tumia dawa za kufubaza VVU     utoro huo umekuwa ukiongezeka siku  hadi  siku  katika Mkoahuu
Dr  Yahaya  Hussein alieleza wataweza  kutowa huduma ya kuzuia  maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto  yaani wamelenga  kuongeza maeneo ya kutolea huduma  kwenye maeneo ambayo hayakuwa na kituo  cha kutolea huduma  hivyo wataoa huduma ya Mkoba
Pia  zitasaidia kusafirisha sampuli  za  damu  (DBS ) toka  sehemu  moja  hadi  nyingine  na  hatimaye zipelekwe  maabara  kubwa ya Mbeya  ilikubaini  maambukizi ya  toka kwa mama kwenda kwa mtoto
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr  Rajabu  Rutengwe  alisema msaada huo uliotolewa  na  shirika la  Walter  Red   Program HJFMRI ni ushahidi tosha kwamba shirika  hilo  linania  njema ya kuisaidia Serikali  hasa  katika Wizara ya Afya  na ustawi wa  jamii
RC alisisitiza  kwamba  pikipiki  hizo   zitumike  kwa ajiri  ya shughuli  za  afya na  hususani  za  Ukimwi na sivinginevyo  na  watumiaji watambue hivyo  si kwa matumizi yao banafsi
Aliwaagiza Wakuu wa Wilaya  na Wakurugenzi kuhakikisha wanawachukulia  hatua  za kinidhamu wale wote ambao watabainika  kutumia  pikipiki hizo kwa matumizi yasiyokusuhudiwa
Mkoa  wa Katavi  unazo  jumla  ya  Halmashauri nne  ambazo  ni  Mpanda  Mjini  Nsimbo , Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Mlele  na Halmashauri  ya  Nsimbo  ambapo kila  halmashauri  imepatiwa  Pikipiki  sita
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa