Home » » HIFADHI YA KATAVI YAKAMATA ZAIDI YA MAJANGILI 40O NA SILAHA ZA KIVITA KWA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA‏

HIFADHI YA KATAVI YAKAMATA ZAIDI YA MAJANGILI 40O NA SILAHA ZA KIVITA KWA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA‏



Na  Walter  Mguluchuma 
Mpanda  Katavi
 Zaidi ya  majangili   400  wamekamatwa  katika  Hifadhi  ya Taifa ya Katavi  wakiwa  na silaha  tano  za  kivita  aina  ya  SMG  na  silaha  aina  ya  G3   pamoja  na   Risasi  357 katika  kipindi  cha  kuanzia  june  2013  hadi  june  2014
Hayo  yalielezwa  hapo jana   na  Mkuu wa  Idara  ya  ulinzi  wa  Hifadhi   ya  Taifa  ya Katavi   Davis  Mushi  wakati  akitoa   taarifa  ya  Hifadhi  ya  Taifa  ya  Katavi  kwenye kikao  cha  kamati ya  ushauri  ya  Wilaya  ya  Mpanda  kilichofanyika  kwenye  ukumbi  wa Idara  ya  maji  Mjini  hapa
Mushi  aliwaeleza  wajumbe wa  mkutano  huo  katika  kipindi   cha  mwaka   2013  na  2014 wamefanikiwa  kukamata majangili  409  wakiwa  na  silaha   za  kivita bunduki  aina ya SMG  tano ,G3 Bunduki  aina  ya   Riffle    nane , Shortgun  21  magobore  138   Bastola mbili   na  Risasi    za   SMG 357
Alisema kuwepo kwa  makazi ya  wakimbizi ya  Katumba  na  Mishamo  karibu  na  Hifadhi kumesababisha  wakimbizi  wa  makazi  hayo  kujihusisha   na shu\ghuli za  ujangili   kama njia  ya kupatia  kipato  chao
 Alifafanua  kati ya  majangili  wanaokamatwa  na  meno ya  tembo  baadhi yao  huwa ni wakimbizi  wanaotoka  kwenye  makambi  hayo  ya  wakimbizi ya  Katumba  na  Mishamo
Alieleza  wakimbizi  toka  kambi  hizo  ndio  waingizaji  wakubwa wa  silaha  za  kivita  kama vile   Smg , G3 ,  Sar na  Ar 15  ambazo  wamekuwa wakizitowa  Nchini  kwao  na  kuzitumia kufanyia ujangili  ndani ya  Hifadhi ya  Taifa  ya  Katavi
Mushi   alieleza   uingizaji  wa  silaha  nyingi  za  kivita  smg  , G3 na Sar  kutoka  Kigoma unafanywa  na  wafanyabiashara  haramu  wa  mano  ya   Tembo  unaofanywa ilikurahisisha  shughuli  za ujangili
Alisema   silaha  hizo zinapoingizwa  hupewa majangili  ili kuwawindia  tembo  au hudalisha  kwa  meno ya  tembo na  silaha  hari ambayo inapelekea  kuzagaa  kwa  silaha nyingi za  kivita  na  majangili  wengi  kwa sasa  wamebadilisha  matumizi  ya  silaha kutoka  magobore  hadi kuwa silaha za kisasa   si kwa kuwindia tembo tuu  hata  wanyama wengine
 Alltaja  sababu  nyingine  zinazochangia ujangili  katika hifadhi  hiyo  ni  kuwepo  kwa mapoli mengi  yasiyo na  ulinzi  hivyo kuwa  ni sehemu ya kujifichia kwa majangili  na pia wanyama wengi  kutoka  hifadhi ya  Katavi  huwindiwa huko  mfano ni msitu  wa  Msaginya
Aidha  magobole  mengi  kumilikiwa kihalali  hari hii inafanya  watu wengi  kumiliki silaha hizo  kwani kibali chake ni shilingi elfu moja  ambapo kazi kubwa ya Magobole  hayo  ni ujangili wa  wanyama  na hasa  Tembo
Pia  kuwepo  kwa silaha  zinazomilikiwa  na watu  kihalali  kama vile bundu  za  aina  ya  Rifle  watu  hao wanamiliki silaha  hizo wamekuwa wakizikodisha  kwa  majangili  wa wanyama  na   hasa  Tembo
Vilevile   kuanzishwa kwa  kwa  vijiji  kando kando ya Hifadhi  na  hasa  ndani ya  mita  500 toka  mpakani mwa  hifadhi  kinyume cha  sheria  ya  wanyama  pori  ya mwaka 2002 hali hii inapelekea  baadhi ya waalifu  kuhamia  kwenye vijiji hivyo  na kuendesha  shughuli za ujangili ndani ya  Hifadhi ya Katavi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa