Home » » NEWS: Majambazi wavamia kambi ya wachina na kumjeruhi mlinzi‏

NEWS: Majambazi wavamia kambi ya wachina na kumjeruhi mlinzi‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399

Na  Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi
Watu  wanane  wanaosadikiwa kuwa  majambazi  wakiwa na siraha za  jadi  mapanga na marungu wamevamia  kambi  ya Kampuni  ya  wachina  wanaotengeneza  Barabarakwa kiwango cha rami  ya kutoka Mpanda   hadi  Sitalike  Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi  na kumjeruhi  mlinzi wa Kampuni  hiyo
Kwa mujibu  wa Kamanda  wa Jeshi  la Polisi  wa Mkoa  wa Katavi Kamishina   mwandamizi  msaidizi   Dhahiri Kidavashari alisema  tukio  hilo  lilitokea  hapo  Aprili 22 mwaka huu  majira ya saa tano  na  dakika  thelathini  na  tano  usiku  katika  kambi ya kampuni  hiyo iliyoko  katika  Eneo  la  kata ya Magamba  Wilaya ya Mlele Mkoa   wa Katavi
Alisema  siku  hiyo ya  tukio  watu hao  wanane  wanaosadikiwa  kuwa  ni  majambazi  walifika  kwenye  kambi  hiyo  na  kisha  walimvamia  mlinzi wa kampuni  hiyoj Joseph     Sarangi     na kumshambulia  kwa kutumia  silaha za  jadi  mapanga  na  marungu  na   kumjeruhi  kwenye paji la uso na  kichwani  kufanikiwa kuiba   betrii  la  gari  aina ya  Nissan  lenye  Namba  120 na kisha kutokomea  kusikojulikana
  Alieleza kuwa  jeshi  la  Polisi  lilipata  taarifa ya  tukio hilo  baada ya  muda  mfupi   baada  ya  kuwalimetokea  kwenye  eneo hilo  na  walianza  wawafatilia  watu hao  waliohusika  na  tukio  hilo  laujambazi  wa  kutumia  silaha   hizo za  jadi
Kamanda Kidavashari alisema  katika msako huo  wa Jeshi  la polisi siku hiyo hiyo   walifanikiwa  kumtia  mbaroni  mtuhumiwa  mmoja  aitwaye  Juma   Athumani  23  Mkazi  wa Mtaa wa Tambukaleli  Mjini  hapa
Alisema  baada  ya  kumkamata  mtuhumiwa  huyo  mmoja  jeshi  hilo  bado  linaendelea  kuwatafuta watuhumiwa   wengine  saba  ambao walishiriki  kwenye  tukio hilo la  ujambazi  wa kutumia  silaha   za  jadi
Aidha  alieleza  kuwa  mtuhumiwa Juma  Athumani  anatarajiwa  kufikishwa  Mahakamani  mara  baada ya upelelezi  wa  tikio  hili  utakapo  kuwa umekamilika  ili sheria  iweze  kuchukua  mkondo wake   wa sheria

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa