WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI YARIDHISHWA NA VYUO BINAFSI VYA UALIMU

Na Walter Mguluchuma, 
Mpanda.

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini imetakiwa kupitia upya sera yake juu ya uendeshaji wa vyuo binafsi vinavyotoa mafunzo ya ualimu nchini ili kuviwezesha vyuo hivyo kutoa taaluma stahili ya ualimu kwa ajili ya kuboresha stadi na elimu kwa wanachuo wanaohitimu kupitia vyuo hivyo.

mkuu wa chuo cha ualimu cha St. Aggrey Chanji kilichopo katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Danford Kabuje alisema hayo jana wakati akisoma  risala kwa mgeni rasmi kaimu mkuu wa mkoa wa rukwa, moshi chang’a, wakati wa mahafali ya kwanza kwa wahitimu wa stashahada na ya pili kwa wahitimu wa daraja la iii a.

alisema kuwa licha vyuo binafsi kuwa  ni sehemu ya wadau wa elimu hapa nchini lakini mfumo uliopo hivi sasa wa kutovishirikisha vyuo binafsi  katika misaada ya hali na mali inayotolewa na serikali kwa vyuo vya umma inavinyima vyuo hivi fursa ya kuinua sekta ya elimu nchini.

Naye,  Mkuu wa wilaya ya Kalambo, Moshi Chang’a alisisitiza umuhimu wa walimu kuzingatia miiko na maadili ya taaluma yao,  sambamba na kuepuka vitendo vinavyosababisha kutokea kwa momonyoko wa maadili katika jamii hivyo kufanya taaluma ya ualimu kudharaulika.

Chang’a alisema kuwa baadhi ya walimu kutofuata maadili na kuzingatia miiko ya kazi yao ndio kiini mmomonyoko wa madilii kwenye kwani wamekuwa na tabia chafu ambazo haziendani na kazi yao hali inayopelekea watoto kuiga tabia hizo pindi wapopelekwa shule kwa lengo kupata elimu.

Aliongeza kuwa hiyo ni changamoto kwa walimu kuhakikisha wanasimamia maadili na miiko ya kazi yao hali itayosaidia kukuza maadili ya watoto nyakati watakazo kuwa shuleni.

Mmoja wa wanachuo wanaohitimu elimu hiyo, Boniventure Ngassa ameitaka Serikali kuhakikisha inaiweka mazingira mazuri ya kujenga miundombinu yatakayowavutia wanafunzi shule za ekondari kuanzia ngazi ya chini kupenda kusoma masomo  sayansi ili taifa lisikose wataalamu wanaotokana na masomo hayo.

WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI YA MIZENGO PINDA WAFANYA FUJO BALAA, WAVUNJA MAJENGO YA SHULE NA NYUMBA ZA WALIMU

Na Walter Mguluchuma,
Mpanda.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mizengo Pinda  kata ya Kibaoni  Wilayani Mlele wamemshambulia kwa mawe na matofali mkuu wa shule hiyo na mwalimu wa taaluma na kuharibu jengo la utawala na nyumba za walimu hao  baada ya kuwatuhumu walimu hao kuwa ni washirikina.
Kaimu kamanda wa poli wa mkoa wa katavi Joseph Myovela alisema tukio hilo limetokea hapo juzi majira ya saa 2:30 usiku
Alisema chanzo cha tukio hilo kilitokana na mwanafunzi mmoja hapo juzi majira ya saa saba mchana kushikwa na ugonjwa wa mapepo uliomfanya aanguke chini
Aalisema wakati akiwa ameshikwa na mapepo hayo aliwataja ALICO Kamyoge (36) ambaye ni Mkuu wa shule hiyo ya sekondari ya Mizengo Pinda na mwalimu wa taaluma Bonifasi Nsalamba (35) kuwa ndio wamemroga ugonjwa huu wa mapepo
Myovela alisema ndipo ilipotimia muda huo wa saa mbili wanafunzi hao walipojikusanya na kuandamana hadi kwenye jengo la utawala na kuanza kulishambulia kwa mawe na matofali na kuweza kuvunja mlango na dirisha la jingo hilo.
Alieleza baada ya kufanya uharibifu kwenye jengo la utawala walielekea kwenye ofisi ya mwalimu wa taaluma ambapo waliharibu mtandao wa mawasiliano kwenye Computer.
Wanafunzi hao ambao muda wote walikuwa na hasira walielekea nyumbani kwa mkuu wa shule huku wakiwa na matofali na mawe walipofika na kumkosa mkuu wa shule aliyekuwa amekwenda kwenye matembezi ya jioni walianza kushambulia nyumba yake kwa mawe na tofali na kuharibu mlango na madirisha.
Kaimu kamanda Myovela alisema kisha kundi hilo lilielekea nyumbani kwa mwalimu wao wa taaluma Bonifasi Nsalamba ambapo walimkuta akiwa anajiandaa kuingia ndani ya nyumba yake akitokea matembezini.
Alieleza ndipo walipoanza kumshambulia kwa mawe katika sehemu mbalimbali za mwili wake huku wakimzomea kuwa mchawi huyo mshirikina walizomea hivyo.
Alisema katika shambulio hilo wanafunzi walimjeruhi mwalimu Bonifasi na kumsababishia majeraha katika mwili wake na aliweza kutibiwa katika zahanati ya kibaoni na kuruhusiwa na hari yake inaendelea vizuri.
Jeshi la polisi mkoa wa katai limetoa wito kwa wanafunzi wa shule hiyo na shule nyingine  za mkoa huo waachane na kuamini imani za ushirikina na polisi inaendelea na uchunguzi  wa tukio hilo ili kuwabaini waliohusika na waweze kuchukuliwa hatua.

JELA MIAKA SITA KWA WIZI WA MILIONI 34

Na Waler Mguluchuma
Mpanda
Mahakama ya hakimu mkazi  ya Wilaya  ya Mpanda  Mkoa  wa Katavi  imemuhukumu Yona   Enerest (42)  mkazi wa   Kijiji  cha Majimoto  Tarafa ya Mpimbwe  kifungo   cha  miaka  sita  jela  kwa  kosa la wizi  wa kuamiwa.
Hukumu   hiyo ilitolewa  hapo juzi na  Hakimu  mkazi    mfawidhi   wa  mahakama ya Wilaya   ya  Mpanda Chiganga  Tengwa  baada ya   kuridhika na  ushahidi ulio tolewa mahakamani  hapo
Awali  mwendesha  mashitaka   Inspekita  msaidizi   Ally Mbwijo  aliiambia  mahakama  kuwa  mshitakiwa  Yona  hapo    April mwaka jana alichukua   jumla  ya    shilingi  milioni 34 kwa  Ismail Salehe  mkazi wa  Mkoa  wa Morogoro  kwa lengo  la kumnunulia  mpunga
Alisema  baada  ya kuwa  amepewa  pesa  hizo  hakununua  mpunga    kama walivyo  kuwa  wamekubaliana  na kila alipo  kuwa akiagizwa   amtumie   mpunga wake  alikuwa akimdanganya  kuwa  eneo  ulipo  mpunga    kunatatizo    la  usafiri  na magari  hayafiki huko
Mwendesha mashitaka Ally Mbwijo  alieleza   kuwa   Isumail  alipo ona  mpunga wake   amechelewa  kuupata  aliamua  kuufuatilia kwa  mshitakiwa  na alipo  ambiwa   amkabidhi  mpunga wake  hata hivyo  mshitakiwa  hakuweza  kufanya hivyo
Hakimu   mkazi   Chiganga  baada ya kusikiliza  uhahidi   ulio tolewa  mahakamani  hapo  alieleza  kuwa mshitakiwa  amepatikana na hatia  ya kujipatia pesa  kwa njia ya udanganyifu  hinyo mshitakiwa  Yona Ernest  amehukumiwa kifungo  cha miaka sita jela na mali zake  ziuzwe  ili  kulipia deni  la milioni 34
Wakati  huo  mahakama hiyo ya Hakimu  mkazi  imemuhukumu  Lubeni  Obedi   (25)  mkazi  wa kijiji  cha  Ilunde  Wilaya  ya Mlele kifungo   cha  miaka mitano  jela  kwa kosa la kuvunja  na kuiba  bidhaa mbalimbali  za dukani
Hukumu  hiyo ilitolewa  na Hakimu  mkazi   mfawidhi   wa mahama ya wilaya  ya Mpanda Chiganga Tengwa.
Mshitakiwa alidaiwa kiiba mafuta  ya taa lita 40,  viberiti  vya chuma  50,  bunda    20 za  sigara  pamoja na pesa tasilimu  shilingi 15,000 mshitakiwa alidaiwa kutenda kosa hilo hapo oktoba 15 mwaka jana

POLISI WAKAMATA KATONI 16 ZA POMBE KALI KUTOKA NCHI JIRANI ZILIZOINGIZWA KINYEMELA

Na Walter Mguluchuma
Mpanda jeshi  la Polisi  Wilaya   ya Mpanda  mkoa wa  Katavi  limekamata  katoni  16 za  pombe  kari  aina ya Vodka  zilizo ingizwa kutoka Nchi  jirani ya Burundi  bila kulipiwa ushuru
Kamanda wa polisi  wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  alisema  pombe  hizo  ziiizo  kuwa zimetokea  Nchi  jirani ya Burundi zilikamatwa  hapo  Aprili  13 mwaka huu majira ya saa  12 jioni katika  maeneo  ya soko  la Bzogwe
Alimtaja aliye  kamatwa na pombe  hizo  kuwa ni  Hadija Hussein (40)  mkazi wa  Mkoa wa  kigoma  aliye  kamatwa  na pombe hizo muda mfupi  baada   ya  kuingia  mjini  Mpanda   akiwa  anatokea  Mkoani  Kigoma kwa  kutumia  basi  la kampuni  ya  Adventure
Alisema Hadija   alikamatwa kufuatia  taarifa  zilizo  lifikia jeshi  la polisi   kutoka  kwa raia  wema  kuwa  anajihusisha  na uwingizaji wa  pombe  karl  kutoka  Nchi  jirani   bila kulipia ushuru.
Kamanda Kidavashari  alieleza   baada  ya jeshi  la polisi  kupata  taarifa hizo   lilianza uchunguzi  wa kumfuatilia  mfanya biashara huyo wa kutokea Kigoma
Ndipo ilipo fikia   siku  hiyo  polisi   waliokuwa  wakiongozwa  na  Operation ofisa  wa jeshi  hilo  wa Mkoa  wa Katavi  Timithi   Nyika  walipo  fanikiwa  kumkamta  mtuhumiwa Hadija  akiwa na katoni  16 za pombe  kari aina ya Vodka
Kidavashari  alisema  mtuhumiwa  anatarajiwa  kufikishwa mahamani  mara  baada ya upelelezi  kuwa  umekamilika   mapema wiki lijalo
Jeshi  la polisi  Mkoa  wa Katavi limetowa  wito  kwa   wananchi   kutoa ushirikiano kwa  polisi  katika kuwafichua wafanya biashara wanao igiza bidhaa bila  kulipia ushuru  na kuisababishia Serikali kukosa  mapato
Baadhi ya  wafanya biashara  wamekuwa  wakikwepa kulipia  ushuru  wa bidhaa   zinazo toka katika Nchi za Burundi    na DRC kwa kupitia mwambao  mwa ziwa Tanganika

KIJANA WA MIAKA 26 JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA KIKONGWE

Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Mahakama  ya Hakimu mkazi ya Wilaya  ya  Mpanda Mkoa  wa Katavi   imehukumu Sindembala Msagi  (26) mkazi  wa  kijiji   cha Bulembo  ya wakimbizi   ya Katumba   wilaya  ya Mlele  kifungo   cha miaka  30 jela   kwa  kosa  la kumbaka  kikongwe  mwenye  umri wa miaka( 90)
Hukumu  hiyo  ilitolewa  jana  na  Hakimu  Mkazi  Mfawidhi  wa  mahakama ya   wilaya   ya Mpanda  Chiganga  Tengwa  baada  ya kulidhika  na  ushahidi  ulio  tolewa  mahamani  hapo  na  pande   wa mashitaka  na utetezi
Awali katika  kesi hii  mwendesha  mashitaka    wa  jeshi  la  polisi  Inspekita  msaidizi Ally Mbwijo  alidai mahamani  hapo  kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo  Desemba  23 mwaka  jana  nyumbani  kwa kikongwe huyo  aliye  kuwa  ana   tatizo la ugonjwa  wa kupoza  mguu na mkono wa kushoto
Mshitakiwa  Sindembala  alidaiwa  siku  hiyo majira  ya saa tano usiku  alikwenda  nyumbani  kwa mama huyo aliye kuwa akiishi  peke yake  na kubomoa mlango  wa nyumba  ya mama huyo   na kisha kuingia ndani
Mwandesha  mashitaka  alieleza  mshitakiwa  baada  ya  kuingia ndani  alimshika  kwa nguvu  kikongwe  huyo  na kuanza kumbaka licha ya mama  huyo kupiga  mayowe  hakuweza  kupata msaada  kwa majirani  kutokana  nyumba  ya mama huyo  kuwa mbali na majirani wenzake
Kikongwe  huyo  alijaribu  kumsihi  mshitakiwa  afimfanyie kitendo  hicho  kutokana  na umri   wa mama huyo  kuwa mkubwa  na tendo hilo alisha liacha  miaka mingi iliyo pita
Alisema mahamani hapo  mshitakiwa  Sindembala  aliombwa na mama huyo  amwache  kumbaka  na akawatafute wanawake  wanao lingana   nae  lakini  mshitakiwa aliendelea  kumbaka   kikongwe bila kujari  uzee wake
Mwandesha mashitaka Ally  Mbwijo  aliendelea  kueleza  mshitakiwa   baada ya  kumbaka  mama huyo  kwa muda mrefu  alijikuta amechoka   na kupatwa  na  usingizi  ulio mfanya  alale  ndani ya chumba cha kikongwe
Ilipo  timia  muda  wa saa 12 alfajiri  mama  huyo alifungua  dirisha  na kumwona mtu mmoja akipita aitwaye Abushola Elly jirani na nyumba  yake  ndipo   alipo mwita kwa ishara  ya vidole  na mtu huyo aliweza  kuitikia wito na  mama huyo  alimwoleza kuwa amebakwa   na aliye mbaka   bado  yumo  ndani  amesinzia
Mtu huyo  ambae alikuwa shahidi katika  kesi hii aliingia  ndani  na kumkuta  mshitakiwa akiwa bado amelela  na baada ya kuwa amemtambua   aliogopa kumkamata  akiwa peke  yake  kutokana  na tabia  aliyo  kuwa nayo   mshitakiwa  Sindembula  ya ukorofi na ugomvi   hari ilyo mfanya akimbie kwende  kuwaita majirani
Mwendesha mashitaka  alieleza   majirani  walipo fika  katika eneo hilo  walimkuta mshitakiwa akiwa  ameondoka   ndipo   wananchi wa kijiji hicho  wakishirikiana na polisi  wa kituo  cha Kanoge  walipo weza kufanikiwa kumkamata mshitakiwa kabla ya kufika nyumbani kwake
Katika utetezi  wake mshitakiwa   aliomba  mahakama imwachie  huru  kutokana   na ushahidi ulio tolewa dhidi yake  kuwa ulikuwa  wa uongo 
Hakimu mkazi mfawidhi  Chiganga  alisema  mahamani hapo kuwa  katika kesi hiyo  ameridhika na  mwenendo mzima wa kesi kwa ushahidi  wa pande hizo mbili  za mashitaka   ambao  ulikuwa na mashahidi  wanne  na mshitakiwa aliye jitetea mwenyewe
Alisema kutokana  na ushahidi  huo mshitakiwa  amepatikana na hatia  ya kuvunja sheria  ya kifungu  namba  154  cha kanuni ya adhabu   cha marekebisho ya mwaka 2002
kutokana kosa  hilo  mahama imemuhukumu   mshitakiwa   Sindembali Msagi  kwenda jela  kutumikia  kifungo cha miaka 30 kwa kitendo chake  cha kumbaka  kikongwe huyo
Mahakama  wakati wa kuisikiliza kesi hiyo  illazimika  huhamia  nyumbani  kwa mama huyo  kusikilizia  kesi  hii kutokana  na kikongwe  huyo kutokuwa na hari nzuri ya kiafya   toka alipo fanyiwa kitendo hicho

WATU WAWILI WAUAWA KWA WIZI WA MBUZI

Na Walter Mguluchuma
Katavi
Watu wawili   wakazi wa  kijiji  cha Matandalani   wilaya ya mlele Mkoa  wa Katavi  wameuwawa na wananchi   baada ya kukili kuiba mbuzi  dume  wa  mwanakijiji  mwenzao
Kamanda wa  Polisi  wa Mkoa  wa  Katavi Dhahiri Kidavashari  aliwataja walio uwawa  kuwa   ni Alex Kazimoto (28) Tonora Luchagula (30)  wote wakazi  wa kijiji   cha Matandalani
Alisema tukio hili  lilitokea  Aprili  14 mwaka huu majira  ya saa saba  mchana ambapo  chanzo  cha  vifo  vya watu hao  vilitokana  na wizi  wa mbuzi  walioiba  hapo  Aprili 10  nyumbani  kwa  Jacob Sekela
Jacob baada ya kugundua  mbuzi  wake dume  ameibiwa  alikwenda  kutoa taarifa  kwa mwenyekiti wa  kijiji  hicho Malcus Wimbi  ambae  nae  aliwapa  jukumu askari   mgambo wa kijiji  hicho  kumtafuta mbuzi   huyo aliye ibiwa
Kamanda Kidavashari  alieleza  ndipo  askari mgambo  walimkamata Tonora Luchagula  na walipo muhoji alikiri  kuiba mbuzi  huyo akiwa  na  marehemu   Alex Kazimoto  na ndipo  mgambo  hao  walipo  wachukua  watuhumiwa   na kuwapeleka  nyumbani  kwa mwenyekiti
Ndipo ilipo timia  saa 2 usiku kundi la  watu lililo jiita Mwano  lilifika  nyumbani  kwa mwenyekiti  na kumwamuru  mwenyekiti awape watuhumiwa  hao  baada  ya   mwenyekiti  kuwakatalia  walianza kumshambulia  na kufanikiwa   kuwatoa watuhumiwa   na kuondoka nao   na walimuonya mwenyekiti asiwafuate  vinginevyo  watamuuwa
Kamanda  alisema  kundi hilo   lilikwenda na watuhumiwa hadi nyumbani  kwa  Donard  Sorera  ambae  ndie  anadaiwa kuwa  ndiye aliye  watuma  kwenda kuiba mbuzi  huoyo walipo mkosa  ndipo  walipoanza  kuwashambulia  wahuhumiwa  kwa kutumia  silaha za jadi   hadi  kufa
Katika tukio hilo  watu  wawili  Deus Zegula  na Malcus Wimbi  wanashikiliwa  na jeshi  la polisi  kuhusiana na   mauwaji  ya watu  hao kwa ajiri  ya maojiano
Jeshi  la polisi mkoa wa Katavi   limetoa wito  kwa wananchi  kutojichukulia  sheria mikononi  na badala yake  watowe ushirikiano  kwa jeshi hilo  kwa kutowa taarifa  ambazo  zitaweza  kuwabaini  watuhumiwa  wanao husika  na matukio  kama haya  ili waweze kukamatwa  na kufikishwa  mbele  ya vyombo   vya dora  na sheria  iweze kuchukua  mkondo wake

WAWILI WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUWAZUIA ASKARI MAGEREZA WASIFANYE KAZI YAO


Na Walter Mguluchuam
Sumbawanga.
JESHI la polisi Mkoani Rukwa  linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuzuia askari magereza kufanya kazi ya kumkamata  Mfungwa aliyetoroka katika gereza za mahabusu la Sumbawanga ,aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka 15 jela baada ya kupatikana na hatia ya unganganyi wa kutumia silaha.
Aidha katika tukio hilo askari wa magereza walimjeruhi kwa risasi  kijana Isiaka  Andrea mwenye(17) ambaye ni mdogo wa mfungwa  aitwae Nizal Paschal alitoroka  kifungo chake mwaka mmoja uliopita baada ya kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani .
Akizungumza na vyombo vya  habari kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa Bw Jacob Mwaruanda amesema kuwa tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika kijiji cha Isesa  kilichopo katika manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa, na kuwataja vijana hao wanaoshikiliwa na jeshi hilo kuwa ni Mosea Andrea(19),Pamoja na Nduguye aitwae Isiaka  Andrea(17) ambaye amelazwa ward namba tatu  ya hospitali ya mkoa  wa rukwa akitibiwa jeraha la risasi lililopo katika mguu wake wa kulia
Akifafanua juu ya tukio hilo kamanda Mwaruanda amesema kuwa inadaiwa  kuwa askari hao waliizingira nyumba hiyo mara baada ya kupata taarifa za siri toka kwa raia wema zilizoeleza kuwa mfungwa aliyetoroka gerezani mwaka mmoja uliopota amerudi na kuungana na familia yake na ndipo siku ya tukio majira ya jioni askari hao wa magereza walifika katika nyumba hiyo kwa lengo la kumkamata kijana huyo ili sheria iweze kuchukua mkono wake.
Alisema kuwa hata hivyo mara baada ya kufika katika nyumba hiyo ndipo vijana hao pamoja na nduguyao ambaye alifanikiwa kutoroka  mara baada yaa kugundua kuwa waliopo nje ya nyumba yao ni askari walitoka wakiwa na silaha za jadi mikononi mwao kwa lengo la kutaka kuwajeruhi askari hao na kwa bahati nzuri askari mmoja alifyatua risasi iliyomjeruhi kijana huyo mguuni.
Kamanda Mwaruanda alisema kuwa mara baada ya vijana hao kuona askari hao wametumia silaha hiyo ndipo walipotupa silaha zao za jadi ambazo ni mapanga mishare na marungu jambo lililofanikisha askari hao kuwakamata huku mfungwa aliyetoroka gerezani akifanikiwa kuwakacha askari hao
Kwa upande wake baba mzazi wa mfungwa huyo aliyetoroka na kusababisha kizazaa kwa familia yake Bw Paschal Andrea  amesema kuwa  majira ya saa sita usiku nyumba yake ilivamiwa na askari magereza saba ambao kwa usiku huo hakuweza kutambua kuwa ni askari kutokanaa na kiza kinene kutanda ,na kisha askari hao  bila ya kufuata taratibu na kufyatua risasi iliyomjeruhi kijana wake,
Alisema kuwa mara baada ya kijana wake kujeruhiwa alianza kupiga kelele za kuomba msaada ndipo mzee huyo ambaye alikuwa amelala  na kuamshwa kwa kelele za risasi alipotoka  na kisha nae kuambulia kipigo toka kwa wajela hao ambao alifanikiwa kuwatoroka muda mfupi baadaye.
Naye Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Isesa   Bw Revocatus Kasuku  licha ya kulaani  kitendo hicho cha kijana huyo kujeruhiwa kwa risasi amesema kuwa kwa kipndi kirefu sasa  watumishi wa jeshi  la polisi wamekuwa wakifika katika kijiji hicho na kuendelea na oparesheni mbalimbali bila ya kuwashirikisha w viongozi wa maeneo hayo.
Bw Kasuku amesme kuwa kutokana na vitendo hivyo kuendelea kwa muda mrefu sasa amekwisha peleka barua ya malalamiko kwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya sumbawanga ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo na anasubiri utekelezaji wake.

WANAFUNZI WA SEKONDARI WAWASHAMBULIA WANAKIJIJI WAKIWATUHUMU KUMUUWA MWALIMU WAO KWA USHIRIKINA


Na Walter Mguluchuma
Katavi
Wanafunzi  wa Sekondari  ya Usevya  Wilayani  Mlele Mkoa wa Katavi  wamezishambulia  familia mbili  kwa kutumia   silaha  za jadi na kuwavunjia nyumba  zao baada  ya kuzituhumu  familia hizo  kuwa zinajihusisha  na  vitendo  vya  kishirikina  uliopelekea kifo   cha mwalimu  wao
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi  Dhahiri Kidavashari  alisema  tukio hili  lilitokea  hapo  juzi  majira  ya  saa  12 alfajiri  baada ya wanafunzi  wa shule  hiyo walipo  pata taarifa  ya kifo  cha mwalimu  wao Tumsifu  Philimon  (28) aliye  fariki  dunia  katika Hospital ya Sumbawanga  aliko  kuwa akipatiwa matibabu  usiku  wa tukio hilo.
Kidavashari  aliwataja   walio  vamiwa  nyumba zao  na wanafunzi  kuwa  ni  Philipo  Mwanjisi  na Aprotina  Mkalala  ambapo  mbali  ya nyumba zao  kuvunjwa   walishambuliwa pia  kwa kupigwa  na mawe
Kabla ya tukio hili  mmoja  wa  familia hizo    alifika  shuleni  hapo  wiki iliyo  pita   kwa lengo  la  kuonana  na  Mwalimu Tumsifu  baada ya kupata  malalamiko  kutoka  kwa mtoto wake  aliye kuwa akisoma hapo  alikwenda  mshitaki mwalimu  huyo  kwa mzazi wake kuwa  amepingwa viboko  na mwalimu Tumsifu adhabu ambayo mzazi huyo hakuridhika nayo
Inadaiwa  baada ya mzazi huyo  kufika  shuleni  hapo  alimpa  vitisho  mwalimu  huyo  huku  baadhi ya wanafunzi  wakisikiza  vitisho vilivyo  tolewa  na mzazi  huyo  wa mwanafunzi
Siku  iliyo fuata  mwalimu  huyo  aliamka  akiwa anaumwa   na ndipo  alipo  amua  kusafiri  hadi  Sumbawanga  waliko  wazazi  wake kwa lengo  la kwenda  kupata matibabu
Ilipofikia April 12  mwalimu huyo alitoweka hospital hadi hapo april 15 ambapo mwili wake uliokotwa akiwa amekufa kando kando ya mto huku akiwa amenyofolewa macho
Kamanda  Kidavashari  alisema   wanafunzi   hao  walihisi  kuwa kifo   cha  mwalimu  wao   kimesababishwa  na kurogwa  na wanakijiji hao  wawili  nandipo  walipo amua  kwenda  kushambulia    wanakijiji hao  na kuvamia nyumba    zao
Alisema upelelezi wa tukio hili  unaendelea  ili kuwabaini  wanafunzi  wote  walio husika  na tikio  hilo  na   watakao bainika waweze kuchukuliwa  hatua
Kwa upande  wake  mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Gemela Rubinga alisema  anategemea  leo  kwenda  shuleni hapo ili kuzungumza  na wanafunzi hao  wa shule  ya Sekondari ya Usevya  ili kubaini   chanzo  cha  vurugu  hizo

AUAWA BAADA YA KWENDA KUOMBA GAZETI LA KUVUTIA SIGARA

Na  Walter Mguluchuma
Mpanda
Jeshi  la polisi  mkoa   wa Katavi  linamshikilia  Albert  Ades (25) mkazi   wa Katandala  Sumbawanga   kwa  tuhuma   za  kumuuwa Yassin Lupinda  (22) kwa kumchoma   na kitu  chenye  ncha  kali  kufuatia  marehemu  kumwomba gazeti  la kuvutia sigara
Kamanda  wa poilisi  wa  Mkoa wa Katavi Dhahiri kIdavashari  alisema tukio hilo  lilitokea Aprili 12 majira ya saa 6 usiku  katika kambi ya uvuvi  wa samaki  ya  mtakuja  Tarafa ya Mpimmbwe Wilayani Mlele Mkoa wa katavi
Alisema  siku  hiyo  ya tukio  marehemu  alikwenda  kuomba  gazeti  la kuvutia  sigara  kwenye kambi   jirani   ya uvuvi  aliyo  kuwa akiishi  mtuhumiwa 
Kidavashari alieleza  baada  ya marehemu  kufika   kwa mtuhumiwa  na  na kueleza  shida yake  ya kuomba  gazeti  la kuvutia  sigara mtuhumiwa  alimweleza  marehemu  kuwa  hayuko  tayari  kumpatia  gazeti  la  kuvutia zigara
Marehemu Yassin aliendelea kumsihi  mtuhumiwa   amsaidie kipande  hata  kidogo  tuu  cha gazeti  kutokana  na kiu  kubwa aliyo kuwa aiisikia  ya  ya kuvuta  sigara
Hata hivyo mtuhumiwa  aliona  kama  imekuwa  kwake   ni kero   kwa marehemu  kuendelea  kumwomba  kipande  cha gazeti   la kuvutia  sigara
Kamanda  Kidavashari  alieleza  ndipo  marehemu  alipo  taka kuchukua  gazeti  kwa nguvu  kitendo   ambacho  hakikumridhisha  mtuhumiwa  Albert
Ndipo  ulipo  tokea  ugomvi  na  mtuhumiwa  alipo   mchoma   marehemu  kwa kitu  chenye  ncha  kali   sehemu  ya  kifua  na kumfanya apige  mayowe  ya kuomba msaada
Majirani  wa kambi   za  wavuvi   walifika  kwenye  eneo  hilo  na  walimkuta  Yassin akiwa  amegalagala  chini  huku  akiwa  amelala kwenye  dimbwi la damu  na walipo jaribu  kumwinua  waligundua  ameisha  kufa  na  wavuvi  hao walifanikiwa  kumkamata  mtuhumiwa muda huo huo
Kamanda  Kidavashari  alisema  mtuhumiwa  anatarajiwa  kufikishwa  mahamani  kujibu  shitaka  la  huhuma   za mauwaji  mara baada  ya    upelelezi utakapo  kamilika

CHUO KIKUU CHA KILIMO KUJENGWA KATAVI

Zaidi  ya Shilingi Bilioni 4.5 zinatarajiwa kutumika kwaajili ya mchakato wa awali wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Katavi , kinachotarajiwa kujengwa mjini Mpanda.

Akizungumzia ujenzi huo Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Mpanda Bw. Joseph Sebastian Mchina amesema kiasi hicho cha fedha kimepatikana ikiwa ni mkopo kutoka benki ya African Trade Insurance Agency (TIA).

Bw. Mchina amesema fedha hizo zitatumika kwaajili ya kulipa fidia ya eneo la ardhi  lenye ukubwa wa hekari mia tano, ambazo zinatarajiwa kujengwa chuo hicho sanjari na gharama za andiko la mradi wa chuo hicho.

Mkurugezni huyo amesema chuo hicho kinatarajiwa kujengwa katika eneo la Kazima nje kidogo ya mji wa Mpanda ambapo katika matumizi ya fedha za awali pia mtaala wa chuo hicho utaandaliwa.

Amesema chuo hicho licha kujengwa mjini Mpanda kinatarajiwa kuwanufaisha wakazi wa mikoa jirani ya Rukwa na  Kigoma ambapo katika hatua za ujenzi wa majengo yake jumla ya Shilingi Bilioni 650 zinatarajiwa kutumika ikiwa ni ruzuku kwa asilimia themanini  na mkopo kutoka kwa Wafadhili kutoka nje ya nchi.

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa